Dkt Magufuli misaada ya wahisani ni mzigo wa miba

justine uwezo

New Member
Nov 24, 2015
1
0
Muheshimiwa Magufuli tumbua mapema majipu ya misaada ya wahisani kwani ni saratani kwa ustawi wa uchumi wetu..

Hakuna msaada wa bure unaotoka kwa wanaojiita wahisani ndo mana licha ya debt relief program ya miaka ya 90 nchi za kiafrika zimeendelea kulipa takribani $ 20 bilioni kwa kila mwaka

Pamoja na misaada hiyo zaidi asilimia 50 ya watu wasiopungua milioni 350 wanaishi chini ya dola moja kwa siku

Kwa wazungu there is no free lunch"yaani hakuna msosi wa bure kila senti moja ya wahisani itarudi kwa kwa njia saba huo ni msaada.?

Misaada mingi imekua shubiri na imetufanya watumwa na kushindwa kujiamulia namna ya kutumia rasilimali zetu..mfano huwezi kua na bargaining power ya kutosha kwenye mikataba muhimu mfano ya madini na gesi ilihali unasaiwa...

Misaada mingi Africa imekua ni ndoano ya watwana kupoka rasilimali za wananchi..

Misaada hii ingekua na tija mbona shilingi inashuka thamani kila kukicha.?pato la mtu mmoja mmoja (per capita income )limekua dogo ukilinganisha na miaka ya sabini...

Uchumi unazidi kudorora na mfumuko wa bei kila leo deni la Taifa linaongezeka ipo wapi tija ya misaada ya wahisani.?

Misaada hii pia imekua chanzo cha rushwa kwa vigogo wa serikali mapema mwaka 2002 umoja wa nchi za Africa ulikadiria rushwa barani Africa inaigharimu dola bilioni 150 kwa mwaka

Usiogope kutumbua jipu misaada mingi haina tija na inatumika kama kigezo cha kua watumwa wa rasilimali zetu wenyewe ndo mana wanatupa na wanakuja kuchukua chao kama collateral sasa huo ni msaada au mzigo wa miba..?

Ipo haja ya kuangalia vizuri eneo hilo
 
Back
Top Bottom