Moshi News
New Member
- Oct 1, 2021
- 1
- 2
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mh. Abbas Juma Kayanda, ameongoza viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kupokea Vyumba vya Madarasa 85 vilivyokamilika kwa asilimia 100%.
Katika Hafla hiyo fupi iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Himo mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Madarasa yote 85 kupitia fedha za UVIKO 19.
Mhe. Dkt Kimei (Mb) amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kupatikana kwa Fedha zote ambazo ni zaidi ya Bilioni 1.7. Kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Vunjo tunasema Ahsante Mhe. Rais kwa Fedha hizi Kwasasa tuna uhakika wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wataenda Shule bila shida. Pia, amewapongeza watendaji kwa ushirikiano wao kufanikisha Kukamilika kwa Mradi huo kwa wakati na ubora Mkubwa.