Dkt. Emmanuel Nchimbi afanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini Tanzania Yordenis

Dkt. Emmanuel Nchimbi afanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini Tanzania Yordenis

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
260
Reaction score
199
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amefanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini Tanzania Mhe. Yordenis Despaigne Vera, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, leo tarehe 12 Machi 2026.

Mazungumzo hayo, yamelenga kuimarisha uhusiano wa muda mrefu wa Tanzania na Cuba, ambao unatimiza miaka 64. Cuba na Tanzania zimekuwa zikishirikiana katika Sekta mbalimbali za kimkakati kama vile Elimu, Afya, Utalii pamoja na Kilimo.

IMG-20260312-WA0140.jpg


Tanzania na Cuba kwa miaka mingi zimeendelea kuwa na mahusiano na maelewano ya kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia katika ngazi ya nchi mbili, kikanda na kimataifa. Tanzania na Cuba zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1962 mara tu baada ya Tanzania kupata uhuru mwaka 1961.

IMG-20260312-WA0133.jpg
IMG-20260312-WA0145.jpg
IMG-20260312-WA0144.jpg
IMG-20260312-WA0139.jpg
 

Attachments

  • IMG-20260312-WA0141.jpg
    IMG-20260312-WA0141.jpg
    333.3 KB · Views: 6
  • IMG-20260312-WA0146.jpg
    IMG-20260312-WA0146.jpg
    315 KB · Views: 3
  • IMG-20260312-WA0137.jpg
    IMG-20260312-WA0137.jpg
    261.9 KB · Views: 3
Vipi hawajazungumza lolote kuhusu Polepole?
 
Trump kesha Cuba is next na ipo karibu sana kufilisika, bila boost au kuungwa US inakufa
 
Back
Top Bottom