Dk. Slaa aacha ombwe CHADEMA

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
Dk. Slaa ambaye ni nadra sana kutofika Makao Makuu ya Chadema Mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam, hajakanyaga eneo hilo wiki nzima sasa na tayari pengo lake limeanza kuonekana.

Pengo la kwanza la Dk. Slaa lilionekana jana wakati wa hafla ya kuchukua fomu za urais kwa aliyekuwa kada wa CCM na Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi wa Richmond, Edward Lowassa.

Lowassa aliyejiunga na Chadema Jumanne ya wiki hii ni mwanachama pekee wa chama hicho aliyechukua fomu za urais hadi jana, ingawa mchakato huo ulikuwa wazi tangu wiki iliyopita.

Baadaye vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) utawashindanisha wawakilishi wa vyama hivyo ili apatikane mgombea mmoja ingawa pia taarifa zilizowahi kuandikwa na gazeti dada na hili, Raia Mwema, ziliweka bayana kwamba Ukawa ujumla wao wamekwishakukubaliana Lowassa awe mgombea wao wa urais.

Raia Tanzania liliwasilli Mtaa wa Ufipa saa nne asubuhi na kukuta watu wakiupamba mtaa huo tayari kwa mapokezi ya Lowassa.

Lowassa aliwasili ofisini hapo mchana, akapokewa na viongozi wa Chadema, huku wanachama waliokuwapo hapo wakiimba: "Tuna imani na Lowassa! Oyaa oyaaa oyaaaa! Lowassa kweeli! Kweeli…"

Kwa mujibu wa taratibu, mtangaza nia huyo alitakiwa kutia saini kitabu cha wageni katika ofisi ya Katibu Mkuu wa Chadema.

Kwa kuwa mwenye ofisi hiyo, Dk. Slaa hakuwepo wala Naibu wake Tanzania Bara; John Mnyika, ambaye ndiye anayeonekana kufanya shughuli nyingi za ofisi hiyo, ilibidi Naibu Katibu Mkuu upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu, ampokee Lowassa.

Hata wakati wa utoaji fomu za urais, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ndiye aliyemkabidhi fomu akisaidiwa na Tundu Lissu pamoja na Mwalimu.

Katika hali iliyoibua maswali mengi, Naibu Katibu Mkuu Bara, Mnyika, hajaonekana hadharani na kazi zake sasa zikifanywa na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Mwalimu, tangu siku ya kutambuliswa kwake katika Hoteli ya Bahari Beach bila kutolewa maelezo ya kina.

Gazeti hili limekuwa likimtafuta Mnyika kutoa ufafanuzi juu ya kutokuwapo kwake katika tukio "muhimu" la kumkaribisha Lowassa na hata kumpatia fomu ya kuwania urais, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda kwani hadi simu zake za mkononi hazikuwa zikipatikana.

Chanzo: Raia Mwema
 
Slaa ana uwezo mkubwa wa kupambana na mafisadi.Namshauri ahamie CCM na Apewe Uwaziri mkuu kwenye serikali itakayoundwa na Magufuli.

Naamini Raisi akiwa Magufuli na waziri mkuu Slaa kitaelweka.Mafisadi lazima wasikie tumbo la kuharisha vichakani watakakokimbilia.
 

Nashindwa kuamini kama hii umepost wewe....! Pamoja na kuwa una mzio na CHADEMA but this is too low for you East African Eagle
 
Last edited by a moderator:

Ccm haikurupuki hata ubaloz wa nyumba kumi hapewi kwanza kadi za wanachama zimekwisha makao makuu labla tumuweke pembeni kama wa akiba ikitokea mtu amefariki tutampatia
 
Chadema wameshauza nafasi ya kugombea urais kwa mgombea binafsi...
 
Huu utakuwa usajiri mzuli na ccm watakuwa wamelamba dume.nape fanyieni kazi fursa hiyo.
 
Huu utakuwa usajiri mzuli na ccm watakuwa wamelamba dume.nape fanyieni kazi fursa hiyo.

Endeleeni kuota ndoto za mchana... giza likiingia tushawapasua..mnajitekenya mnacheka wenyewe mnataka na ss tucheke, hizi story za kufirika endeeleni nazo, kasema punde mtaficha sura zenu, ogopa mtu anasifia jambo ambalo halipo wala Dr. Hana wazo lio wazo..mwaka huu mtashika adabu hakika!!
 
Duh.movie bado inaendelea siiasa za Bongo bhana pasua kichwa kweli
 
nani mmiliki wa gazeti Raia Tanzania???....sitashangaa ikiwa ni Zitto Kabwe
 

Na bado, mbona mtaweweseka sana mwaka huu!
 
Vikao vya maandalizi ya cc ya Chadema vinaendelea kwa nguvu kubwa, ambapo Katibu Mkuu Dr Slaa anaongoza jopo hilo akiwa na Naibu Katibu Mkuu Mh Mnyika, na Mwenyekiti Wa Bawacha Halima Mdee,
Dr Slaa amesema kuwa porojo zinazoendelea katika magazeti hazina msingi na mda ukifika wazushi hao wafiche sura zao.

Katika hatua nyingine Dr Slaa amesema kuwa baada ya mkutano mkuu kupitisha jina la Lowasa kuwa Mgombea rasmi, hafla ya kumtangaza itafanyika uwanja mkuu wa kisasa Dar es Salaam uliopo Temeke.

Amewaomba wanachama wa chadema wote kuwa watulivu pia wanaukawa wote kuwa wamoja mpaka ccm iondoke.

Pipooooooozzziii!!
 
Mmmmm!
Mbona hatuelezwi kwanini hajaonekana hadharani katika matukio yote yanayomhusisha Lowasa.
Dr. bado ana maadili ya dini hawezi kukubali kirahisi kumeza maneno yake mwenyewe, labda tu Lowasa atubu mbele ya watanzania asamehewe ndipo atakaa meza moja na Dr. Slaa. 'Time will tell' na haya maneno yangu mtayakumbuka.
 

hujielewi wala huelewi unachokizungumzia ndugu-hivi unajua Itafaki? M/kiti anaweza kumkabidhi mgombea Urais kwa misingi kuwa Katibu ana kazi nyingne? acha porojo
 

Weye hauna Bakulutu uko Petit Frere, mambo kani hii unasema hauna bien
 
Ndiko hua kina kitila wanaandika makala zao huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…