Diwani wa Vingunguti, Mhe. Omari Saidi Kumbilamoto ni mfano wa kuigwa

Sep 29, 2016
34
83
OMARI S KUMBILAMOTO DIWANI BORA AIGWE NA VIONGOZI WA KISIASA NA SERIKALI

Anaandika Mwl Razaq Mtele Malilo

Leo January 8-2017 nilihudhuria mkutano wa hadhara wa diwani wa Kata ya VINGUNGUTI ambaye pia ni naibu mstahiki meya wa manispaa ya ILALA kwa tikiti ya CHAMA CHA WANANCHI CUF MHE OMARI S KUMBILAMOTO hii ni kutokana na kuona juhudi zake kupitia mitandao ya kijamii na hivyo ikanifanya nivutike kwenda kumuona.
Nimeona juhudi zake na mambo aliyoyafanya MUBASHARA na jinsi gani wananchi wake walivyo na furaha kupata diwani mchapakazi.
Kwa juhudi zake hizo inanifanya niseme kuwa OMARI KUMBILAMOTO si tu kuwa ni moja kati ya madiwani bora nchini bali pia ni moja kati ya viongozi makini anayefaa kuigwa na kila mmoja.
Nisiongee mengi, soma ni nini Mhe Omary Kumbilamoto amefanya ndani ya mwaka huu mmoja ndani ya kata yake ya VINGUNGUTI.

MAMBO ALIYOYATEKELEZA MHE OMARI SAIDI KUMBILAMOTO NDANI YA MWAKA MMOJA KATIKA KATA YAKE YA VINGUNGUTI YENYE WAKAZI 82,169 NA IDADI YA KAYA 21,868. MAELEZO HAYA YAMETENGWA KWA SEKTA

1. SEKTA YA AFYA

katika sekta MHE KUMBILAMOTO amefanikiwa kufanya vitu vifuatavyo:-

(a) Amefanikiwa kupeleka vitanda viwili vya kujifungulia akina mama katika Zahanati ya kata ya VINGUNGUTI hivyo ameweza kutatua kero hiyo kwani Zahanati hiyo ilikuwa na vitanda viwili ambavyo vilikuwa havitoshi na chakavu.

(b) Amefanikisha upatikanaji wa Gari la kubebea wagonjwa wa dharula (AMBULANCE) ambayo ilikuwa ni kilio kikubwa cha wakazi wa VINGUNGUTI

(c) Amefanikisha upatikanaji wa baiskeli ya kubebea wagonjwa waliozidiwa katika Zahanati ya kata ya VINGUNGUTI

(d) Amefanikisha kujenga choo kimoja ndani ya wodi ya wazazi.

(e) Amefanikiwa kununua GENERETA moja kwa ajili ya Zahanati ya VINGUNGUTI ili kuepuka kadhia ya giza pindi umeme ukatikapo.

(f) Amefanikiwa kupeleka feni 4 ambazo zimefungwa katika Zahanati ya VINGUNGUTI

(g) Amefanikiwa kupeleka TV moja katika Zahanati ya VINGUNGUTI kwa lengo la kuwezesha wafanyakazi/wauguzi na wagonjwa kupata habari mbalimbali juu ya nchi yetu na dunia kwa ujumla.

(h) Amepeleka mashine ya kufulia nguo na mashuka ya wagonjwa katika Zahanati ya kata kwa lengo la kuondoa usumbufu kwa wafanyakazi wa Zahanati hiyo.

(i) Amefanikiwa kupeleka mashine za kupimia presha na kisukari lengo ni kuwasaidia wanaohitaji huduma hiyo kwa ukaribu zaidi.

(j) Amefanikiwa kupeleka tochi kama mgonjwa ana tons.

(k) Amepeleka panzia yanayotumika hospitalini kuzungushia kitanda ambacho kuna mgonjwa aliyezidiwa sana ama kufariki kabla ya utaratibu mwingine kuchukuliwa.

(k) Amefanikiwa kupanua maabara ya Zahanati ya kata ya VINGUNGUTI

2. SEKTA YA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI

(a) Ametoa mashine ya kuzalishia nyaraka (printer) katika SHULE YA SEK YA VINGUNGUTI

(b) Amelipa deni la umeme la Tsh 500,000 Katika shule ya msingi ya MIEMBENI ambapo deni hilo lilipelekea shule hiyo kukosa umeme kwa mwaka mzima.

(c) Kwa kushirikiana na manispaa ya Ilala amefanikiwa kumaliza tatizo la madawati katika shule zote ndani ya kata yake.

3. SEKTA YA MICHEZO

(a) Ametoa jezi seti 14 katika timu za mipira wa miguu na vikundi vya mazoezi ya asubuhi (jogging)

(b) Ametoa vifaa vya mabondia katika vikundi vya vijana wa kazikazi.

4. SEKTA YA UTUMISHI WA UMMA

(a) Muundo wa kata ya Vingunguti imeundwa na Mitaa sita. Katika kuboresha ufanisi wa utendaji kazi na utoaji huduma kwa wananchi wa kata ya Vingunguti, watendaji na wenyeviti wanahitaji kuwa na ofisi nadhifu za kufanyia kazi mitaa yote na kwa kuanzia MHE KUMBILAMOTO AMEKARABATI OFISI YA KATA/OFISI YA DIWANI

5. MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII NA VIJANA

(a) Amewezesha uchimbaji wa mifereji ya maji katika mtaa wa BUTIAMA ambapo kazi iliyobaki ni kuujenga tu.

(b) Amefanikiwa kutekeleza ahadi yake ya kurudisha taa za barabarani kwenye njia ya kwenda machinjioni na MIEMBENI

(c) Ametimiza ahadi yake kwa wazee wa VINGUNGUTI kwa kuwawekea sola katika kijiwe chao cha kahawa maeneo ya relini.

(d) Amepeleka tank la maji lita 5000 katika mtaa wa KOMBO

JAMBO MUHIMU KABISA

Manispaa ya Ilala imepanga kutoa mikopo kwa vikundi 5,420 kwa wanawake na vijana kwa manispaa mzima katika mwaka wa fedha 2016/2017 zimetengwa Tsh Bilioni nane milioni mia sita na sitini (8,660,000,000/=) kwa ajili ya kutoa mikopo kwa makundi ya vijana na wanawake.
Kwa kata ya VINGUNGUTI mpaka sasa manispaa ya Ilala imetoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi vya vijana na wanawake wapatao 75 ambao tayari wamepatiwa mkopo toka DCB BANK.
HII YOTE NI CHINI YA USIMAMIZI NA UFUATILIAJI WA DIWANI MAKINI NA NAIBU MEYA WA ILALA MHE OMARI SAIDI KUMBILAMOTO

HITIMISHO

MHE Omar Kumbilamoto licha ya mafanikio hayo anatambua changamoto nyingi zinazoikabili kata yake na kuahidi kuto bweteka na kuwatumikia wananchi kadri ya uwezo wake ili kutatua kwa pamoja kero za wananchi wa kata hiyo.

Nawaomba viongozi wote kufanya kazi ya kujitoa zaidi ili kuwatumikia wananchi kwani mmewekwa hapo ili kuwatumikia wananchi kwa kuwaongoza kwa ushirikiano wa pamoja ili kutatua kero zao na kuwasaidia kupata maendeleo.

IMEANDIKWA NA NDUGU MWL RAZAQ MTELE MALILO

Email mtelemwalimu@gmail.com

Simu
0659913056
0763753832
0625568417

VIVA OMARI SAIDI KUMBILAMOTO, USIBWETEKE PIGA KAZI KUWATUMIKIA WANANCHI MPAKA SIKU YAKO YA MWISHO
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom