Diwani kata ya Mtibwa ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 14

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,735
22,433

Morogoro. Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Diwani wa kata ya Mtibwa wilayani Mvomero (Chadema), Lucas Edward (38) maarufu kwa jina la Mwakambaya kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 14 mkazi wa Turiani wakiwa katika nyumba ya kulala wageni.

Kamanda Ulrich Matei alisema jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa msiri wao kwamba katika nyumba hiyo ya kulala wageni kuna mtu ameonekana akiwa na binti mdogo ndipo askari walipofuatilia nyendo zake na kumkamata.

Alisema askari baada ya kufika katika nyumba hiyo ya kulala wageni ya Baraka walimkuta mtuhumiwa huyo akiwa na binti huyo chumbani na kwamba uchunguzi wa kitabibu unaendelea ili kubaini uhalisia.

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya Mvomero, Mrisho Ramadhani alikiri kukamatwa kwa diwani huyo na kwamba mpaka sasa hajafahamu kosa alilokamatiwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Huu ni uongo uliotukuka. Haiwezekani kamanda Lucas Mwakambaya afanye ufyatu kama huu! hili ni zengwe na mpishi mkuu ni manyang'au wa CCM.
Ngoja nifuatilie kwa karibu ntaleta mrejesho.
 
Hii habari sio ya kweli.
Muda huu nimetoka kuongea diwani wa CHADEMA kata ya MTIBWA mh LUCAS MWAKAMBAYA.
Kiufupi tu; Mh Diwani kalaani sana juu ya hizi tuhuma, si za kweli hayupo kizuizini wala hafikirii kama itatokea hivyo katika mazingira yoyote ya haki.

Mleta mada tafadhari sana, naomba uweke tarehe na toleo la hilo gazeti au walau weka picha iliyosheheni hizo taarifa ili tuweze kubaina ni nani alizusha upuuzi huu.

Moderator; tafadhari futa huu uzi make hauna chembe ya uhakika hata kidogo.
 
Huu ni uongo uliotukuka. Haiwezekani kamanda Lucas Mwakambaya afanye ufyatu kama huu! hili ni zengwe na mpishi mkuu ni manyang'au wa CCM.
Ngoja nifuatilie kwa karibu ntaleta mrejesho.
Hata mimi nimeshangaa mwakambaya? Figisu figisu za mahamba hizii huyu diwani ni tishio
 
Hata mimi nimeshangaa mwakambaya? Figisu figisu za mahamba hizii huyu diwani ni tishio
Nakuhakikishia hakuna kitu kama hiki, hizi ni figisu za Vanzeeland baada ya kuona moto wa Mwakambaya ni hatari kwake.
Ikumbukwe kuwa Jonas Van-Zeeland ni diwani wa Diongoya(kapita kwa pingamizi) na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero[alipita baada ya kuwahonga madiwani wote hasa wa ccm ambao ni wengi(kutokana na ufinyu wa uelewa wa watu wa huko). Aliwapa mlungula kwenye tour ya Mikumi].
Hata hivyo, Van zeeland anashirikiana bega kwa bega na Mbunge wa Mvomero Sadik Mulad(kanjibai masikini) std VII ambaye ana hali tete ya kiuchumi na kesi ya rushwa ndani ya utumishi wa BUNGE!

Ikumbukwe kuwa Mulad alifulia sana sema zeeland kambeba kwa kuingiza vibasi uchwara kwenye kampuni.
Watahangaika sana ila Watashindwa!
Kamwe Mwakambaya hatikiswi na hatatikisika mpaka awe Mbunge wa Mvomero.
 
Diwani wa Mtibwa wilayani Mvomero, Lucas Edward (38) maarufu Mwakambaya anashikiliwa na Polisi Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 14, mkazi wa Turiani kwenye nyumba ya kulala wageni.

Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Ulrich Matei alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 29 saa 12 jioni kwenye nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Sultan, Manispaa ya Morogoro.

Matei alisema polisi walipata taarifa kutoka kwa msiri wao kwamba katika nyumba hiyo, kuna mtu ameonekana akiwa na binti mdogo, hivyo askari walifuatilia nyendo zake na kumkamata.

Alisema askari baada ya kufika kwenye nyumba hiyo, walimkuta mtuhumiwa huyo akiwa na binti huyo chumba namba 108.

Alisema uchunguzi wa kitabibu unaendelea kuthibitisha tuhuma hizo.

Akizungumza kwa simu, Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Mvomero, Mrisho Ramadhan alithibitisha kukamatwa kwa diwani huyo na kwamba mpaka sasa hajafahamu ni kwa tuhuma gani.

Ramadhan alisema kwa sasa wao kama viongozi wa chama wanafuatilia kujua tuhuma na ameomba uongozi wa Chadema Mkoa kufuatilia zaidi na kwamba, atatoa taarifa baada ya kufahamu kwa undani.

“Ni kweli nimesikia mheshimiwa kakamatwa huko mjini Morogoro, sijajua kosa nimewaomba viongozi wa Mkoa Chadema kufuatilia nitatoa maelezo baadaye,” alisema Ramadhan.

Alisema baada ya kupata undani wa tukio hilo, atatoa taarifa ili kujulisha umma kilichotokea.
 
Ndio wanataka nchi hawa,kama wameanza kubaka vitoto vidogo hvi,wakipewa nchi itakuaje?

Mtuhumiwa hajui kama.anatuhumiwa maana yuko uraiani na hajakamatwa na polisi.Hata muichukie hiyo CDM lakini hatutaikubali CCM kamwe
 
Diwani wilayani Mvomero,Lucas Edward (38) maarufu Mwakambaya anashikiliwa na Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 14,mkazi wa Turiani kwenye nyumba ya kulala wageni.

Alikamatwa tarehe 29,May saa 12 Jioni,alimbaka binti huyo katika gesti iliyopo mtaa wa Sultani Mjini Morogoro katika chuma namba 108 kwa mujibu wa RPC wa Morogoro Ulrich Matei

Katibu wa Chadema wilaya ya Mvomero Mrisho Ramadhani kathibitisha kukamatwa kwa Diwani huyo.

Nawasilisha.
 
Hii habari sio ya kweli.
Muda huu nimetoka kuongea diwani wa CHADEMA kata ya MTIBWA mh LUCAS MWAKAMBAYA.
Kiufupi tu; Mh Diwani kalaani sana juu ya hizi tuhuma, si za kweli hayupo kizuizini wala hafikirii kama itatokea hivyo katika mazingira yoyote ya haki.

Mleta mada tafadhari sana, naomba uweke tarehe na toleo la hilo gazeti au walau weka picha iliyosheheni hizo taarifa ili tuweze kubaina ni nani alizusha upuuzi huu.

Moderator; tafadhari futa huu uzi make hauna chembe ya uhakika hata kidogo.
Wapi TCRA?
 
Hilo gazeti mwananchi ni la tarehe ngapi ili tukathibitishe au tupate mahali pa kuanzia kuhusu habari hii. Maana kuna ubishani hapa.
 
Back
Top Bottom