kimsingi habari za gazeti la Nipashe,kwa sehemu kubwa zimepotoshwa wala sielewi lengo ni lipi.Ni kweli diwani wa kata ya Ramadhani Njombe alipigwa na kujeruhiwa vibaya na mtu mmoja ambaye ni katibu mwenezi wa kata ya Ramadhani na kwamba tukio hilo lilitokea jirani na ofisi za CCM wilaya ya Njombe ambako diwani alikwenda salon kwa ajili ya kunyoa nywele.Kisa cha mgogoro kati yake na Bwana Ngole ambaye alikuwa kampeni meneja wake wa udiwani 2010 bado hakijulikani ila ugomvi hausiani na nafasi ya uchaguzi ndani ya wilaya.Bwana Ngole hajagombea hata cheo kimoja ngazi ya wilaya.Sasa mwandishi wa Nipashe amepata wapi habari zinazotaka kukwepesha ukweli?Kwa bahati nzuri mimi nimefanikiwa kupata mkanda wa video ambao unaonyesha jinsi diwani alivyofanywa.
Pamoja na yote.Nampa pole sana rafiki yangu Mhe.Alfred Luvanda,mmiliki wa shule ya Livingstone.Mungu amsaidie apate nafuu mapema.Ikumbukwe kwamba huyu diwani amelelewa katika vyama vya upinzani tangu akiwa mdogo.Kwa bahati mbaya sana ameingia mlango wa kutokea.CCM ni chama mfulisi na kuchapana makonde ni jadi yao.Tuko tayari kumpokea tena kwenye harakati za ukombozi wa Njombe yetu.Vua gamba vaa Gwanda kamanda Luvanda.Mwandishi wa Nipashe hajatutendea vema.
Hakuna sababu ya kuficha mambo yanayotokea ndani ya CCM.HATA RADIO NJOMBE IMEGOMA KABISA KUTANGAZA HABARI HIZI.KWA NINI?KUNA LUKANI VAYAWE.
*Pia wamo Samia na
Diwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Ramadhani, Wilaya ya Wangingombe mkoa wa Njombe, Livingstone Luvanda, ambaye alijeruhiwa vibaya kwa kupingwa na mgombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi wa wilaya hiyo, amehamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Fulghence Ngonyani, akizungumza na NIPASHE jana alisema diwani huyo amehamishiwa katika hospitali hiyo kutoka Hospitali ya Mkoa ya Kibena alikokuwa amelazwa awali.
Mgombea huyo ambaye anagombea nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wilaya ya Njombe (jina tunalihifadhi), alimpiga diwani huyo kutokana na misuguano ya kiasa kwa madai kuwa diwani huyo alikuwa kikwazo kwake ili asiweze kuchaguliwa ambapo sasa anashikiliwa na jeshi la polisi.
Awali diwani huyo akizungumza na gazeti juzi akiwa amelazwa katika Hospitali ya Kibena, alisema alivamiwa majira ya saa 5:30 asubuhi wakati akitoka nyumbani kwake kuelekea katika Shule ya Kimataifa ya Mchepuo wa Kiingereza ya Livingstone kuhudhuria mahafali.
Luvanda alisema akiwa hatambui kinachoendelea, ghafla alivamiwa na mgombea huyo na kuanza kumpiga kwa kutumia stuli hali iliyomfanya aanguke chini na kupoteza fahamu papo hapo.
Luvanda alisema kabla ya kupata mkasa huo, alidai mgombea huyo alimtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) katika simu yake ya mkononi akimweleza kuwa nilazima atamuua kutokana na kumuwekea vikwazo ili asichaguliwe katika nafasi anayoomba.
Hata hivyo, wakati tunakwenda mitamboni, taarifa zilizopatikana zilieleza kuwa mgombea huyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe kwa kosa la kumjeruhi diwani huyo ambapo amerudishwa mahabusu baada ya kukosa wadhamini hadi Oktoba 2, mwaka huu kesi hiyo itakaposikilizwa tena.
CHANZO: NIPASHE[/QUOTE]