Diwani CCM aliyejeruhiwa sasa ahamishiwa Muhimbili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani CCM aliyejeruhiwa sasa ahamishiwa Muhimbili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mboko, Sep 27, 2012.

 1. M

  Mboko JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 1,067
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  [h=2][/h]  *Pia wamo Samia na Dk. Mwinyi
  Diwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Ramadhani, Wilaya ya Wanging’ombe mkoa wa Njombe, Livingstone Luvanda, ambaye alijeruhiwa vibaya kwa kupingwa na mgombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi wa wilaya hiyo, amehamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Fulghence Ngonyani, akizungumza na NIPASHE jana alisema diwani huyo amehamishiwa katika hospitali hiyo kutoka Hospitali ya Mkoa ya Kibena alikokuwa amelazwa awali.

  Mgombea huyo ambaye anagombea nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wilaya ya Njombe (jina tunalihifadhi), alimpiga diwani huyo kutokana na misuguano ya kiasa kwa madai kuwa diwani huyo alikuwa kikwazo kwake ili asiweze kuchaguliwa ambapo sasa anashikiliwa na jeshi la polisi.

  Awali diwani huyo akizungumza na gazeti juzi akiwa amelazwa katika Hospitali ya Kibena, alisema alivamiwa majira ya saa 5:30 asubuhi wakati akitoka nyumbani kwake kuelekea katika Shule ya Kimataifa ya Mchepuo wa Kiingereza ya Livingstone kuhudhuria mahafali.

  Luvanda alisema akiwa hatambui kinachoendelea, ghafla alivamiwa na mgombea huyo na kuanza kumpiga kwa kutumia stuli hali iliyomfanya aanguke chini na kupoteza fahamu papo hapo.

  Luvanda alisema kabla ya kupata mkasa huo, alidai mgombea huyo alimtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) katika simu yake ya mkononi akimweleza kuwa nilazima atamuua kutokana na kumuwekea vikwazo ili asichaguliwe katika nafasi anayoomba.

  Hata hivyo, wakati tunakwenda mitamboni, taarifa zilizopatikana zilieleza kuwa mgombea huyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe kwa kosa la kumjeruhi diwani huyo ambapo amerudishwa mahabusu baada ya kukosa wadhamini hadi Oktoba 2, mwaka huu kesi hiyo itakaposikilizwa tena.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Nasikitika sina email ya tendwa, ningemfowadia ajisomee!!!
   
 3. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Bora wampeleke India maana hapa hatuna CT scan hata dawa za ANAESTHIA hatuna akifa watasema tumemua kwa sababu ya mgomo, dawa nyingi tulizonazo feki!!! Halafu mtu mdogo sana kwenye chama. hatutaki lawama
   
 4. D

  Dislike Senior Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu Mboko kata ya Ramadhani ipo Wilaya ya Njombe sio Wanging'ombe.
   
 5. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,201
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Sasa kuna sababu gani ya kuhifadhi jana lake kama mtu ameshafikishwa mahakamani? Mbona washtakiwa wengine wanapigwa picha na kuweka kwenye front pagesa za magazeti na TV? Au Mwandishi amenunuliwa? Mr. Luvanda pole sana lakini anaweza kutuambia lile sakata la mtoto aliyeuawa bwenini kwenye shule yake liliishia wapi?
   
 6. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kumbe mapigano ya kupigania uongozi yapo CCM na siyo CDM.......Propaganda kitu kibaya sana!Ukweli utawaumbua mchana kweupe:rockon:here we go!
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  john tendwa mbona yupo kimya?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. i

  iseesa JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tendwa hajaona "TENDA" hapo hivyo kapotezea
   
 9. MANI

  MANI Platinum Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Mkuu jogi kwani hata hilo nipashe yeye halisomi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Tendwa upo? Tuanze kukifuta kwanza kipi mzee SSM au CDM? Ukipiga kura kwa wananchi, kitafutwa kwanza SSM? Kura kubwa 2015.
   
 11. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  mani, nia yangu ni kumfahamisha kuwa niliidharau kauli yake ya kutishia kukifuta chadema, hivyo asome gazeti la nipashe kwenye email yake kupitia kwangu, na wakati wowote akifikiri kwa kutumia akili za watu ajue tunam-dis huku kitaa.
   
 12. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Pole zake huyo diwani. Haya majitu utafikiri yalizaliwa na madaraka! Je mpaka muda huu polisi hawajamtia nguvuni huyo mhalifu? Hao ndio watu waliojaa CCM.

  Tendwa ni mchumia tumbo mbaya sana. Ishu hizi kwake huwa hazimuusu
   
 13. l

  lutondwe Senior Member

  #13
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kimsingi habari za gazeti la Nipashe,kwa sehemu kubwa zimepotoshwa wala sielewi lengo ni lipi.Ni kweli diwani wa kata ya Ramadhani Njombe alipigwa na kujeruhiwa vibaya na mtu mmoja ambaye ni katibu mwenezi wa kata ya Ramadhani na kwamba tukio hilo lilitokea jirani na ofisi za CCM wilaya ya Njombe ambako diwani alikwenda salon kwa ajili ya kunyoa nywele.Kisa cha mgogoro kati yake na Bwana Ngole ambaye alikuwa kampeni meneja wake wa udiwani 2010 bado hakijulikani ila ugomvi hausiani na nafasi ya uchaguzi ndani ya wilaya.Bwana Ngole hajagombea hata cheo kimoja ngazi ya wilaya.Sasa mwandishi wa Nipashe amepata wapi habari zinazotaka kukwepesha ukweli?Kwa bahati nzuri mimi nimefanikiwa kupata mkanda wa video ambao unaonyesha jinsi diwani alivyofanywa.
  Pamoja na yote.Nampa pole sana rafiki yangu Mhe.Alfred Luvanda,mmiliki wa shule ya Livingstone.Mungu amsaidie apate nafuu mapema.Ikumbukwe kwamba huyu diwani amelelewa katika vyama vya upinzani tangu akiwa mdogo.Kwa bahati mbaya sana ameingia mlango wa kutokea.CCM ni chama mfulisi na kuchapana makonde ni jadi yao.Tuko tayari kumpokea tena kwenye harakati za ukombozi wa Njombe yetu.Vua gamba vaa Gwanda kamanda Luvanda.Mwandishi wa Nipashe hajatutendea vema.
  Hakuna sababu ya kuficha mambo yanayotokea ndani ya CCM.HATA RADIO NJOMBE IMEGOMA KABISA KUTANGAZA HABARI HIZI.KWA NINI?KUNA LUKANI VAYAWE.  *Pia wamo Samia na
  Diwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Ramadhani, Wilaya ya Wanging’ombe mkoa wa Njombe, Livingstone Luvanda, ambaye alijeruhiwa vibaya kwa kupingwa na mgombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi wa wilaya hiyo, amehamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Fulghence Ngonyani, akizungumza na NIPASHE jana alisema diwani huyo amehamishiwa katika hospitali hiyo kutoka Hospitali ya Mkoa ya Kibena alikokuwa amelazwa awali.

  Mgombea huyo ambaye anagombea nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wilaya ya Njombe (jina tunalihifadhi), alimpiga diwani huyo kutokana na misuguano ya kiasa kwa madai kuwa diwani huyo alikuwa kikwazo kwake ili asiweze kuchaguliwa ambapo sasa anashikiliwa na jeshi la polisi.

  Awali diwani huyo akizungumza na gazeti juzi akiwa amelazwa katika Hospitali ya Kibena, alisema alivamiwa majira ya saa 5:30 asubuhi wakati akitoka nyumbani kwake kuelekea katika Shule ya Kimataifa ya Mchepuo wa Kiingereza ya Livingstone kuhudhuria mahafali.

  Luvanda alisema akiwa hatambui kinachoendelea, ghafla alivamiwa na mgombea huyo na kuanza kumpiga kwa kutumia stuli hali iliyomfanya aanguke chini na kupoteza fahamu papo hapo.

  Luvanda alisema kabla ya kupata mkasa huo, alidai mgombea huyo alimtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) katika simu yake ya mkononi akimweleza kuwa nilazima atamuua kutokana na kumuwekea vikwazo ili asichaguliwe katika nafasi anayoomba.

  Hata hivyo, wakati tunakwenda mitamboni, taarifa zilizopatikana zilieleza kuwa mgombea huyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe kwa kosa la kumjeruhi diwani huyo ambapo amerudishwa mahabusu baada ya kukosa wadhamini hadi Oktoba 2, mwaka huu kesi hiyo itakaposikilizwa tena.
  CHANZO: NIPASHE[/QUOTE]
   
Loading...