DIT na UDSM vyatengeneza mfumo kutabiri matetemeko ya ardhi

fungi

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,539
4,672
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kupitia Idara yake ya Uhandisi wa Umeme na Mawasiliano kwa kushirikiana na Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT), wamefanikiwa kutengeneza mfumo wa kutabiri matetemeko ya ardhi yanayotokea nchini.

Mhadhiri Msaidizi wa UDSM, Eva Shayo alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mfumo huo ambao unasaidia katika maeneo ya Magharibi – Kusini mwa Tanzania mfano mkoa wa Mbeya.

Alisema mfumo huo tayari unafanya kazi, pia una lengo la kuendelea kuweka vifaa vingi ambavyo vitasaidia kuangalia matetemeko kwenye mikoa yote iliyopitiwa na bonde la ufa.

“Pia mfumo huo utasaidia watu wanaoishi kwenye hayo maeneo ambayo yana hatari ya kupata matetemeko kuboresha majengo ili yanapotokea nyumba zao zisipate madhara,” alisema.

Alisema kuna kihisio cha bei nafuu ambacho kinatumiwa na watu wanaoishi kwenye hayo maeneo pamoja na kompyuta ambazo zimeunganishwa intaneti ili kutuma kile ambacho kitasomwa na hicho kihisio kwa ajili ya kuchunguza kama tetemeko litatokea.

Shayo alisema katika eneo husika, tetemeko likipatikana wananchi wataarifiwa muda mfupi kabla ya kutokea ili wachukue hatua stahiki.

Alisema mfumo huo ulianza mwaka 2005 baada ya kutokea tetemeko kubwa mkoani Mbeya, lakini tokea wakati huo mpaka sasa hawajapata taarifa ya kuwepo kwa tetemeko lingine. Hapa Tanzania matetemeko yapo ila yanatokea kwenye mikoa ambayo imepitiwa na bonde la ufa kama Rukwa, Kyela(Mbeya), Arusha, Ruvuma na mingineyo.
 
Back
Top Bottom