Dirisha jingine la maombi ya udahili-UDSM

Dirisha jingine la maombi ya udahili-UDSM

mchumi tumbo

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2018
Posts
832
Reaction score
996
DIRISHA JINGINE UDSM:

CHUO kikuu cha Dar as Salaam kitafungua dirisha jingine la maombi udahili kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Elimu ya juu mwaka huu.

Akizungumza katika kipindi cha Jambo kinachorushwa na shirika la Utangazaji Tanzania @tbchabari, Naibu Makamu Mkuu Taaluma, Prof. Bonaventure Rutinwa amesema hadi sasa chuo kikuu cha Dar es Salaam kimeshadahili wanafunzi #7600 hivyo baada ya kikao cha Jana kati ya UDSM, TCU na Waziri Prof. Ndalichako, Sasa UDSM itatakiwa kudahili wanafunzi kulingana na uwezo wake mama ambao ni takribani wanafunzi #15000, idadi ambayo ni karibu Mara mbili ya waliodahiliwa.

Aidha dirisha hili la udahili ambalo litafunguliwa kwa siku nne hadi tano (taarifa kamili itatoka) litagusa programu zote #92 za Chuo hicho huku mwombaji akitakiwa kuomba chuo pasipo matumizi ya codes kama ilivyokuwa ikifanyika siku chache zilizopita na TCU.

Aidha dirisha hili litawahusu wanafunzi ambao;

1. Walikosa vyuo
2. Walipata tabu kutokana na changamoto za confirmation codes
3. Waliomba UDSM lakini kutokana na changamoto mbalimbali wakathibitisha vyuo vingine

Sasa wataomba nafasi hiyo kwa kuzingatia vigezo ambavyo chuo kikuu cha Dar es Salaam kinahitaji!

Katika hatua nyingine Prof. Rutinwa amezungumzia hali ya Taaluma ya Chuo na kusema kwamba hali ni nzuri ukitizama katika msimamo wa ubora wao vyuo kidunia ambapo UDSM kinafanya vizuri kusini mwa jangwa la Sahara.

Aidha kuhusu Malazi, amesema hali siyo mbaya sana, kwani serikali imejenga hostel za Magufuli huku wakiwa katika mkakati wa "tendering " kukarabati Hall 2&5

C&P
 
Washaanza kuleta siasa zao kwenye vyuo,,,

Nahisi Hiki kipindi ndo utakuta mtu mwenye div 1 ya 9 alikosa civil udsm alafu utakuta watoto wa viongozi wenye div 3 ndo watapelekwa wengi sana kujaza hizo nafasi
 
Hilo lipo hata 1st round,kuna dogo alikuwa anatwo ya 10 alipata 1st round MUHAS ila wenye one zao kali wengi waliliwa vichwa
 
Aidha dirisha hili litawahusu wanafunzi ambao;

1. Walikosa vyuo
2. Walipata tabu kutokana na changamoto za confirmation codes
3. Waliomba UDSM lakini kutokana na changamoto mbalimbali wakathibitisha vyuo vingine

Sasa wataomba nafasi hiyo kwa kuzingatia vigezo ambavyo chuo kikuu cha Dar es Salaam kinahitaji!

Hapo kwa marangi ndiyo naona sintofahamu itakapo tokea kwani wanasema hata kama umeconfirm chuo kingine sasa ni ruksa kuomba UDSM na ukichaguliwa poa. Ni wazi kwamba sasa kuna upendeleo wazi wa chuo chetu pendwa. Ingawa hii inaweza kuwa njema kwa wanafunzi wahusika lakini naona mfumo walioleta TCU na serikali kuchafuliwa, kuleta manung'uniko (vyuo vingine) na kwa wale walio kuwa na mkopo kuna uwezekano wa kuingilia upelekaji wa mikopo. Na je mwakani nani atawaamini tena. NAFIKIRI TENA KUNA HAJA YA KUUPITIA MFUMO UNAOTUMIKA NA KUWEKA MAMBO SAWA. Hata mimi huenda nikajaribu kupata nafasi chuo chetu pendwa raundi hii ya nne.
 
Hapa naona mamlaka zinatoa "assist" kwa chuo pendwa kucheza rafu dhidi ya kanuni za mchezo.
 
Nitashangaa kama wataendelea kuleta wanafunzi 15 elfu bila kuboresha/kurekebisha miundombinu.Mfano kama Duce first year walikuwa wanafanya shift kwa masomo ya general.sasa wakiongezwa hawa 15 elfu hali itazidi kuwa mbaya.Nadhani wajaribu na kupanua miundombinu.itafaa zaidi
 
Back
Top Bottom