Dira ya Taifa dhidi ya dira za watawala

dunguni

Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
41
Reaction score
95
Ni kosa kubwa kimaendeleo hasa kwa taifa kuishi kwa maono na dira za viongozi waliopo madarakani, kwa upande mmoja zipo faida hasa pale unapokuwa na kiongoz aliyejitoa kutumikia watu ila madhara yake ni makubwa hasa pale unapokuwa na Taifa lenye mfumo wa uongozi wa miaka mitano hadi kumi.

Ukiwa na mazingira haya utagundua kiongoz anapoondoka na yale yote aliyoanzisha yanakufa maana anayefuata alazimishwi kwa namna yoyote ile kusimamia ya mtangulizi wake.

Ni vigumu na haitokaa itokee kwa taifa lolote linalotumia mfumo wa vipindi viwili vya utawala kunufaika kimaendeleo kwa kuongozwa na dira za watawala bali taifa lolote litakalotaka kusonga mbele lazima likubali kumlazimisha mtawala kusimamia dira iliyowekwa kwa maslahi ya wote.

Mataifa yetu yanakwama si kwamba hatuna viongozi wenye dhamira ya dhati, bali tunakwama kwasababu hao viongozi wenye nia tunaowachagua hawajawekewe mifumo ya kuwadhibiti wasiongoze kwa utashi binafsi bali waongoze kwa kuzingatia dira ya Taifa.

Mfano kwa Tanzania, tumeongozwa na marais watano ila ukiuliza mtu mmoja mmoja kuwa kila rais alifanya nini cha kukumbukwa kwenye afya,Elimu,miundombinu,utalii,uwekezaji na ukuzaji wa uchumi kila utakayemhoji atajibu kwa mrengo wake wa siasa.ILA kati ya sekta zote sekta ya miundombinu iliyojengewa msingi na Mzee Mkapa ndio sekta pekee yenye muonekana wa dira ya Taifa ila sekta nyingine zote zimekuwa zikiyumba kwa sababu kila mtawala anataka kuongoza kwa utashi wake.

Tuangalie sekta ya Elimu ambavyo imekuwa ikichezewa na inaendelea kuchezewa kila kukicha, hakuna anayetaka sekta hii iendeshwe kwa misingi ya sheria bali kila mwana siasa anapopata nafasi anasimamia kile anachoona kinafaa.Sekta hii ilishambuliwa kwa kasi sana mwaka jana tukadhani mikakati ya kitaifa itaweka lakini hadi sasa tunapoangalia speed yote imekwisha na hakuna mabadiliko ya kudumu yaliyowekwa. Tumewatoa wataalam wengi ndani ya sekta hii na kuwatupa nje kwa maelezo kwamba wameshindwa kwenda na kasi yetu lakini hali ilivyo ni kwamba hata hawa wapya nao kasi imewaacha nyuma mile kadhaa....tusimamie maandishi siyo utashi wa mtu

Sekta ya afya nayo ilipokelewa kwa kasi hadi mageti ya wizara yakawa yanafungwa watumishi wachelewaji wanabanwa na kwamba huduma za afya zitaboreshwa.Kwa sababu hatukuwa na dira ya taifa katika sekta hii, sasa hivi matamko yote yamekwisha na kilichobaki nikulaumiana huku huduma za afya katika vituo mbali mbali zikiwa hazikidhi viwango.Turudi kwenye misingi ya taifa kuhusu afya...

Kilimo nako panaendelea kutetereka kwa sababu hakuna misingi ya taifa dhidi ya sekta hii, yapo wapi matrekta yaliyoingizwa nchini kwa maelfu kutekeleza kilimo kwanza? Kipo wapi kilimo kwanza? Kipo wapi kilimo ni uti wa mgongo?Yapo wapi Mashamba darasa ya kilimo kwanza?Kipo wapi kilimo cha umwagiliaji?Turudi kwenye dira ya taifa juu ya kilimo kuwasaidia asilimia 80 ya watanzania waliojikita humo.

Vipo wapi viwanda vya matunda tanga na morogoro? Vipo wapi viwanda vya ngozi vya kusaidia kukuza sekta ya ufugaji?vipo wapi viwanda vya nguo kwa wakulima wa pamba? Turudi kwenye Sera ya taifa juu ya viwanda

Mifugo tuliyonayo na faida zitokanazo na mifugo hiyo ni vichekesho, wenzetu Comoro wanachagua mbegu nzuri ya NGO' mbe na kupeleka kwao kwa ajili ya ufugaji wenye tija, je upo wapi mkakati wa kuboresha ranchi zetu na kuwaelimisha wafugaji kufuga kisasa?Ukifuatilia mawaziri wengi waliopewa sekta ya mifugo wanavyojadili ufanisi wao utakachosikia ni idadi ya migogoro ya wakulima na wafugaji aliyotatua,je mawaziri hawa uteuliwa kwenda kutatua migogoro au kuboresha sekta hii?Dira itatusaidia kuweka maeneo ya kipaombele ...

Hii ni mifano tu ya sekta ambazo zinaathari chanya kwa msisimiko wa uchumi wa taifa letu ila hazina dira inayosimamiwa.....
TUSIMAMIE MAANDIKO YA KITAALAMU YALIYOFANYIWA UTAFITI ILI TUWEZE KUPIMA UFANISI WA WATAWALA WETU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…