wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,932
- 4,542
Ukifuatilia kwa makini kabisa maandiko matakatifu kuanzia Biblia hadi Quran utaona kuwa hakuna kifungu chochote au aya yoyote ambayo inamwelezea Yesu au mtume Mohammed kujihusisha na siasa.
Yesu na mtume Mohammed hawakuwahi kabisa kuhubiri dini na siasa.
Walifanya kazi moja tu ya kuhubiri neno la Mungu. Leo hii maaskofu na masheikhe kila kukicha ni kujikomba Kwa kila serikali inayoingia madarakani.
Hata manabii Kama Isaya na Eliya hawakuwa na muda na siasa za enzi zile, tena waliwapinga wafalme dhahiri kabisa hawakuwaogopa hata kidogo,wao walimwogopa Mungu wa kweli tu.
Leo hii kiongozi wa dini anapelekewa magari kumi ya kumkamata kisa kaikosoa serikali, anafunguliwa kesi akitoka huko anaanza kuipamba tena serikali ile ile aliyokuwa akiikosoa.
Nabii Eliya alimwomba Mungu na kuifungia mvua Kwa miaka mitatu kipindi kile mfalme alipokuwa kiburi, yeye akaenda kujificha porini na huko huko Mungu akawa anamtuma kunguru kumpelekea mikate. Mtumishi akiwa kanisani au msikitini mara unashangaa kaacha kuhubiri neno la Mungu na kisha anaanza kuhubiri siasa.
Kwa kawaida watumishi wa kweli Wa Mungu huwa Hawana urafiki na wanasisa na Watawala, maana mara nyingi Sana Watawala hawatendi haki.
Lucifa tayari ameshaingilia kazi ya Mungu, mnadhani Shetani ni mjinga awaangalie tu eti mnaitafuta pepo wakati yeye anasubiria kusulubiwa Jehanamu, hawezi kukubali ni lazima ahakikishe anaenda kuzimu na wengi.
Nyie mnaojiita watumishi Wa Mungu, chagueni siasa au kumtumikia Mungu full stop.