Dini hudumaza wanafunzi, Wizara ya Elimu China yasema

thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,827
4,757
Serikali katika mkoa wa Gansu, China imeagiza wasimamizi wa shule kutekeleza kikamilifu marufuku ya kutokubalia shughuli zozote za kidini shuleni.

Wizara ya elimu katika mkoa huo uliopo kaskazini mashariki kwa nchi hiyo imechukua hatua hiyo baada ya msichana mmoja kuoneshwa kwenye video akikariri vifungu kadha vya Koran katika shule moja.

Shule hiyo imeshutumiwa vikali na maafisa hao wa wizara ya elimu.

Wizara hiyo kupitia taarifa imesema dini shuleni huathiri hali ya kiakili ya watoto.

Baadhi ya shughuli za kidini hukubaliwa nchini China lakini hudhibitiwa vikali.

Serikali huwa makini sana kuhusu baadhi ya shughuli za kidini ambazo zinaweza kuathiri utambulisho wa kitamaduni wa Kichina.
================
A heavily Muslim Chinese province has demanded strict adherence to a ban on religion in schools after a video circulated online in which a kindergartener recites verses from the Quran.

The government in the northwestern province of Gansu reiterated the officially atheistic communist government's rules forbidding the presence of religion in public schools at all levels, saying it was protecting children.

"This video has drawn a gasp from the public, as many people are infuriated," said a statement issued Thursday. "The Education Department of Gansu province strongly condemns the act that harms the mental health of the youth, and demands education agencies of all levels to stop it resolutely and strictly bans religion from campuses."

In the video, the unidentified girl is seen wearing a black Muslim head covering and sitting in a classroom with dozens of other students — apparently all in Muslim attire.

There is no indication when and where the video was taken, but the provincial government statement said it was taken in the predominantly Muslim prefecture of Linxia. The government did not identify the kindergarten or if anyone from the school was punished.

China also enforces tight restrictions on religious participation by young people outside of school, particularly in its culturally distinct western regions where Islam and Tibetan Buddhism are widely practiced.

The government is especially wary of what it sees as the use of religion to promote a non-Chinese cultural identity or independence for Tibet and the northwestern region of Xinjiang.


Source: AFP
 
Mtoto anakaririshwa mpaka basi....ila darasani anatoka kapa .....tukubali tu duniani nako kuna maisha ingawa ya mpito na huwezi kupata ajira kwa kigezo cha kukariri bibilia Au Koran!
 
Binafsi bado sikubaliani na swala la kuwapo kwa vipindi vya dini shuleni naona ni kuongeza mgawanyiko wa kijamii kwa kiwango kikubwa kabisa maana hizi dini mpka sasa zimeonesha kuleta mgawanyiko kuliko umoja kwenye jamii kuanza kuzijenga kwa ngazi ya shule ni kuongeza huo mgawanyiko
 
Dini huwafanya watu kujiona bora kuliko wengine.

"I know the truth, you don't. I'm lucky and special"

kikifika kipindi cha religion shule, kila kundi linaonea huruma wenzake.

Dini zibaki huko huko, mbali na shule.
 
Binafsi bado sikubaliani na swala la kuwapo kwa vipindi vya dini shuleni naona ni kuongeza mgawanyiko wa kijamii kwa kiwango kikubwa kabisa maana hizi dini mpka sasa zimeonesha kuleta mgawanyiko kuliko umoja kwenye jamii kuanza kuzijenga kwa ngazi ya shule ni kuongeza huo mgawanyiko
Mkuu uwepo wa vipindi hivi ni muarobaini wa maadili na mwenendo mwema, vipindi hivi huongeza hofu Ya Mungu na kupunguza vitendo vya kihalifu na visivyo na maadili.
 
Dini imebaki Africa tu ndiyo tumejazwa imani. Yani staki hata kuskia kuhusu dini mimi zimenipatia vikwazo vyingi katika mahusiano baina yangu mimi na wapenzi niliokuwa nao awali..

Mimi naimani na Mungu tu sio vinginevo.
 
Katika mtizamo wa Kanisa Katoliki Dini ina faida zifuatazo:
1. inafundisha ukweli hasa ule ambao kwa akili zetu hatuwezi kuufikia
2. ni chanzo kikubwa cha amani, upendo, umoja, furaha kwa wengi.
3. inasaidia sana kukuza maadili ktk jamii
4. inatetea wanyonge na hasa masikini
5. inatoa huduma nzuri za kijamii kama huduma za afya, elimu n.k
6. inamsaidia mtu kumjua Mungu na kuungana nae
7. inamsaidia mtu kuwa na matumaini
8. inamsaidia mtu kutambua utu wake, wa wenzake na kuutunza, kuuthamini na kulinda uhai wa viumbe hasa wa binadamu.
9.inasaidia mtu kufika mbinguni.
Nakiri kuwepo kwa matatizo lukuki yanayojitokeza ktk mwamvuli wa kidini ila si sababu za kuiondolea hadhi. zipo dini nyingi kwakweli zinapumbaza watu hilo liko wazi na hata mimi siungi mkono mtu kuwa na dini yoyote tu bali dini ya kweli inayoendana na matashi ya Mungu na isiyopingana na sheria ya asili yaani NATURAL LAW!
 
Mkuu uwepo wa vipindi hivi ni muarobaini wa maadili na mwenendo mwema, vipindi hivi huongeza hofu Ya Mungu na kupunguza vitendo vya kihalifu na visivyo na maadili.
Unaweza kuwa sahihi kwa hiki unachosema lakini faida tunayodhani kuwa tunaipata ni ndogo ukilinganisha wigo mkubwa tunaoutengeneza kwenye jamii pamoja na uwepo huu wa hivi vipindi mmomonyoko wa maadili umeendelea kuwa mkubwa mashuleni
 
hii ni kweli maana hata ukiangalia wafia dini wengi hapa jukwaani ni watu wenye uwezo mdogo wa ku reason,

mijadala yao imetawaliwa na matusi tu bila hata hoja halafu wanajidai wao ndio wasafi
 
Mtoto anakaririshwa mpaka basi....ila darasani anatoka kapa .....tukubali tu duniani nako kuna maisha ingawa ya mpito na huwezi kupata ajira kwa kigezo cha kukariri bibilia Au Koran!
Acha hizo, biblia haikaririwi, ni somo kama psychology inavyofundishwa ;we sema hiyo dini inayokariri usiogope
 
Madini duniani kote haswa Africa ni majipu yanohitaji kutumbuliwa upesi ili kuokoa bara letu na upunguni
 
Madini duniani kote haswa Africa ni majipu yanohitaji kutumbuliwa upesi ili kuokoa bara letu na upunguni
Kwani dini zinatatizo gani ambalo halipatikani kwa njia nyengine zaidi ya kwenye dini tu?
 
Back
Top Bottom