KERO Dimbwi hili barabara ya Tabata Segerea ni shida, mvua ikinyesha inakuwa kero kupitika, mamlaka zipo kimya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
427
Reaction score
666
Sisi Wakazi wa Tabata Segere kwa Bibi tuna changamoto ya Barabara ambayo inaelekea Hospitali ya Segerea, kuna dimbwi kubwa la maji ambalo linazuia wapita njia, pikipiki, na magari madogo kupita. Magari makubwa tu ndiyo yanayoweza kupita angalau yakiwa na uhakika hayatapata tabu sana.

Your browser is not able to display this video.
Hali hiyo tumesharipoti Serikali za Mtaa lakini hakuna kinachofanyika, tunapata athari kwa biashara mvua ikinyesha, maji machafu yanaingia ndani ya fremu za biashara, jambo linalosababisha wafanyabiashara kufunga maduka yao kwa kukosa wateja na uharibifu wa mali.

Barabara hiyo ni muhimu kwa sababu inatumiwa na magari ya wagonjwa (Ambulance) na wajawazito wanaoelekea hospitalini, lakini sasa imekuwa hatari kwani watu wanadumbukia kwenye maji.

Tulitoa taarifa Serikali ya Mtaa tangu mwezi wa tisa Mwaka 2025 lakini wanatuambia suala hilo liko mikononi mwa mhandisi (engineer) bila hatua zozote kuchukuliwa hadi sasa.
 
CCM ina watu wajinga sana, eti mama hana deni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…