Dili la Qatar la $21Bilioni kwa Marekani kusonga mbele licha ya marumbano ya kidiplomasia

Gomez Luna

Senior Member
Mar 13, 2017
187
205
Mpango wa kuuza ndege vita chapa F15 unaonekana kusonga mbele licha ya baadhi ya nchi kukata uhusiano wa kidiplomasia na Qatar kufuatia kile walichokiita kuunga mkono ugaidi.

Idara ya mambo ya nje ya Marekani imeeleza kwamba mzozo wa kidiplomasia na ukosoaji wa Rais Trump dhidi ya Qatar kwa kuunga mkono ugaidi hayajaathiri dili la kuuza ndege vita 72 chapa F-15QA lenye thamani ya dola bilioni 21 kwa Qatar.

Kwenye taarifa yake Boeing imeeleza kwamba inafatilia kwa karibu sana maendeleo ya hivi karibuni kuhusu makubaliano ya ndege hizo ambazo zinatengenezwa na Boeing.
Pia imeongeza kwamba inafanya kazi kwa karibu sana na serikali za Marekani na Qatar kuhakikisha kwamba makubaliano hayo yanafikiwa. Boeing iliendelea kueleza kwamba "Tuna tegemea kwamba makubaliano hayo yatatiwa saini"

ze kokuyo Nalendwa izzo Root
 
Naona inapokuja kwenye hela kila kitu kinawekwa pembeni. Haya marumbano bwana yana kitu nyuma yake. Sasa Trump anasema anataka kuwa mediator kuwapatanisha, baada ya kuonyesha kabisa kuwa anaunga mkono upande mmoja.
 
Back
Top Bottom