Digital Music Changer: Jinsi ya kupata muziki wa quality ya CD kwenye gari lako bila kubadilisha radio inayokuja na gari

RugambwaYT

JF-Expert Member
Jan 11, 2014
1,383
1,852
Digital music changer ni kifaa kinachokuwezesha kutumia media kama USB Flash drive na 3.5mm audio jack kwenye radio ya gari lako na kupata muziski mzuri bila kuibadilisha radio inayokuja na gari. Wengi wetu tumebadilisha radio hizo na kufanya muonekano wa gari usiwe wa kuvutia saana kulinganisha na muonekano wa gari pale linapobaki na radio yake. Shida ni kwamba radio za gari ni za kizamani. Nyingi zinacheza CD yenye nyimbo za WMA, ukiweka mp3 zinagoma.
Kwa vile tunapenda muziki, wengi hubadilisha radio, wachache hutumia FM transmitter kwa ajili ya kusaidia kupata muziki wanaopenda wao.

Kwenye video hapo chini, mdau ameonesha step by step installatio kwa gari aina ya Altezza. Lakini najua hizo devices zinapatikana kwa gari nyingi.
 
Je mafundi wote wa radio wanaweza funga hiyo kitu?
Nafikiri. Maana haiitaji ujuzi wowote zaidi ya ujuzi wa kufungua na kurudisha redio. Kikubwa ni kujua radio yako ina socket ya plug ya cd changer ya namba gani. Kwa Toyota mara nyingi ni 5x7 au 6x6
 
Back
Top Bottom