difference btn RWANDA and ISRAEL against tz...

Hivi kwa nini hamfikirii kumaliza mgogoro na Rwanda kwa njia ya mazungumzo ? Mpaka sasa sijaona juhudi zozote za maana za kidiplomasia kumaliza mgogoro huu kwa njia ya mazungumzo...!

Kagame hataki mazungumzo, ameahidi kwa kumwabia JK 'I WILL HIT YOU'. Sasa hapo kuna mazungumazo tena.
 

mawazo ya watu dhaifu kama wewe ndiyo yanayoleta taifa legelege linalochezewa kama tambara bovu kama inavyofanyika drc, unafikiri nyerere angekuwa na mawazo kama yako migodi ya dhhahabu kule kanda ya ziwa si ingechezewa na hawa jamaa zako kama wanavyofanya drc, isipokuwa misingi aliyoacha nyerere ndio tunafaidi matunda yake na hawa maadui wameshaona kuwa tume-dilute misingi ile kwa mawazo dhaifu yaliyojaa woga na wasiwasi kama yako ndio maana wanaanza kukohoa kwa tz. Vita si lelemama lakini ikibidi lazima ipiganwe!!!!!
 
iNAWEZEKANA, LAKINI NI WAPI UNAWEZA KU-QUESTION POST WAR MANAGEMENT YA TZ? TOKA UGANDA WAR, LIBERATION STRUGGLE ZA ZIMBABWE, MSUMBIJI, SA, COMORO NK
 
Msilinganishe Rwanda na Israel! Ni kuidharau Israel. Tofauti ni kubwa kama mbingu na ardhi!
 
Hivi kwa nini hamfikirii kumaliza mgogoro na Rwanda kwa njia ya mazungumzo ? Mpaka sasa sijaona juhudi zozote za maana za kidiplomasia kumaliza mgogoro huu kwa njia ya mazungumzo...!
kati ya Rwanda na Tanzania nani unadhani ndie hataki mazungumzo?
 
There's long way to go maana MONUSCO wanapigana na M23 na Kagame anaweza kuruka uzi kwamba hahusiki na uadui mkubwa kati yetu na Rwanda ukaendelea wakati huo M23 washasambaratika na MONUSCO hawahusiki tena.
 

Hivi jamani tumerogwa?waliowengi wanajua vita ni kati ya majeshi na majeshi.....kikinuka hapa utajuta ulikuwa unashabikia utumbo....naamini JK hawezi chukulia mawazo kama haya na ndo maana katuma jopo kigali kwa ajili ya kuzungumza haya mambo kidplomasia...kila mwenye busara na kujua nini maana ya amani hawezi shabikia vita...
 

Kaburu, kweli wew upeo wako wa kufikiri mdogo sana, kukataa vita si udhaifu ila umuhmu wa vita hiyo, na wew ni kati ya watu mizigo katika taifa hili.. nyie ndo mnafanya maamuzi kuangalia athari zake, huyo Nyerere unamsema naye kachangia sana tu matatizo ya leo, jiulize 1961 tulipopata uhuru tulikuwa nchi ya kwanza kwa usafirishaji mazao ya kilimo nje, leo ni wangapi??? hivi unajua hasara tuliyopata kutokana na vita vya uganda??? vita si sifa ila sababu na faida ya vitu hivyo ndo muhmu..

Mmarekani si mjinga kutovamia north korea ana uwezo huo ila angalia faida gani ipo korea, DRC imesaidia na Namibia, Angola, Zimbabwe na Libya kuondoa hao waasi kwa miaka bila mafanikio, utasikia wametulia ila baada ya muda wataanza tena, DRC tatizo lipo ndani ya serikali yake yenyewe na viongozi wake na ni suala la kihistoria ambalo haliitaji vichwa vepesi vya kushabikia kama ufanyavyo wewe..!! ungekuwepo kipindi cha mwalimu ungeweza jua athari ya vita ila kwa sababu ya utoto nakushauri kasome uiemike then rudi uchangie
 

Nakubaliana na wewe kuwa vita haijawahi kuwa na gharama ndogo, ila sikubaliani nawe kuwa hasara watu kumwaga damu unavyoilinganisha na kushindwa kusafirisha mazao ya kilimo nje ya nchi wakati gharama yake ni kubwa sana, unaweza usiwe na vita lakini ukashindwa ku export vile vile. jiulize ni vita gani tulikuwa nayo watanzania mpaka tukashindwa kutumia fursa ya mpango wa AGOA kuexport to the largest market in the world, US, at preferential terms? Faida za kiuchumi kuwa na DRC ni kubwa, hivi sasa Kenya, Uganda na Rwanda wameamua kuachana na bandari ya Dar, lakini biashara na Eastern DRC, Zambia, Malawi and I am told even Zimbabwe are increasing to the tune the decision won't affect us as it was thought. can't u see the economic viability of this? China is the coming world economic giant after US, ana business Tz and DRC and someone anataka ku-interupt, nanyi mnakaa kimya kwa kuwa kuna gharama ya vita, that is cowardness! Kuhusu Namibia, Zimbabwe na Angola kuwa ziliwahi kutoa msaada DRC, ni kweli na zilisaidia hawa waasi wasiichukue Kinshasa, without them we could have been speaking other situation now. Lakini unakumbuka TZ kipindi hicho ilirudisha majeshi yake yaliyokuwa kule yakifundisha na haikujiunga na alliance ya Zimbabw, Angola na Namibia? Kumbuka hao ni SADC na kila baada ya operation kuna Post war analysis, je ni kitu gani kinakufanya uamini kuwa haijanyika?
 

Kaburu, sas umeongea.. lakini suala la Malawi kutumia bandari yetu sana ni uongo , hawa jamaa wanapita Msumbuji na walishajitoa zamani na hata wafanya biashara toka Congo wanakimbilia kwa wingi huko tafuta economic report ya World bank utaona.. Zimbabwe wanatumia south africa ni cheap na karibu, kikubwa tunachoweza fanya ni kupunguza rushwa na urasimu pale bandarini na si kujipa moyo hata kidogo..tusiwe taifa la waimba ngonjera na matendo hakuna..

Leo unaongelea kuondoka kuwa wazalishaliji na wasafirishaji mazao Africa wa kwanza kabla na baada ya uhuru na sasa kuwa mkyani, hii ni kwa sababu ya sera mbovu za serikali ya kwanza na Mwalim kutoshaurika na ndo aina ya viongozi na tulionao na pengine wabaya zaidi.. tuzidi kuomba Mungu labda tutapata mtu mwenye akili wa kututoa kuliko ni aibu kushabikia gas na mchina wakat madini yameondoa bila kutunufaisha..

Hivi huyo mchina anafanya nini tofauti na mmarekani?? wote hawa ni wanyonyagi tena mchina ni mbaya zaidi ila wa africa wanampenda hasa viongozi maaana yeye anachojali ni maslahi yake na si utawala bora kama wale wengine.
 
Kinachomuuma Dictator kagame ni Tanzania kupeleka majeshi DRC kuichapa M23. pia anamtegemea kaka yake Dictator Museveni,
 
Nadhani tunawapa kichwa tu Rwanda, hawana chochote cha kuitisha Tanzania, tunapoteza nguvu tu kuijdili Rwanda.
 

Waambie ukweli hao na wakiona unapingana nao wanasema Mara wewe Si Mzalendo Mara wewe Si Mtanzania! Vita Si Mchezo, Hawa wote wanao tamani vita wameshiba! Na wasifikiri Kama vita ikitokea basi tutapigana Rwanda peke yake, kwani kutakua na mataifa mengine yakiisapoti Rwanda! Na ikumbukwe kua maadui wa Tanzania wamejitokeza leo katika uzinduzi wa gati kule Mombasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…