DHL is NO Longer Express

Mwana Kwetu

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2011
Posts
652
Reaction score
610
BIG WARNING!!!!!!!

Kama huko nyuma ulikuwa una import parcel zako toka nje kwa kutumia DHL express Mail unatakiwa ufikirie upya na u switch kutumia mfumo mwingine kama UPS, EMS, au Expedited mail service nyingine lakini Si DHL.

DHL is no longer express mail service kwani kwa sasa ni wakala wa TRA na imepoteza maana ya kuwa express. Unatumiwa mzigo kutoka nje hata wa dola 5 , unafika ofisi za DHL Dar- es- Salaam unakaa pale wiki nzima ukichunguzwa kama bei ya kifurushi ni ya kweli au ya kudanganya. Ikibidi Mzigo utafunguliwa(hili ni zoezi la siku nne) na TRA kwa usimamizi na DHL bila kujali mteja alilipia express mail ili apate mzigo wake haraka.

Kwa ufupi DHL sio option nzuri ya kusafirisha mzigo kama unataka kupata mzigo wako kutoka nje kwa haraka. Ninaandika kwa sababu evidence zipo ambazo hata DHL hawawezi kuzikataa kuwa kuna mizigo zinakaa hadi mwezi mmoja bila kuwa delivered na nina evidence kutoka kwa marafiki zangu wawili.
Ili kuepuka disappointment just tumia means nyingine nilizozitaja hapo juu hazina usumbufu kama DHL.
Nakuhakikishia mzigo wako ukisafirisha kwa DHL utapekuliwa, utafunguliwa kutoka kwenye package simply ni kodi inatafutwa wakati kuna mamilioni yanapotea kupitia mikataba mbalimbali na hata Escrow. Mtanzania naagiza saa tu ya dola 10 basi ni taabu kwani itakadiriwa kutegemea na afisa wa TRA anavyojisikia na inaweza kwenda hadi dola 30 ili wapate kodi wanayotaka.

DHL lazima wajipambanue kama wao ni wakala wa TRA au shirika la kusafirisha mizigo la sivyo litajikuta limekuwa kitengo cha TRA cha kukusanya kodi na hivyo kushindwa kutimiza jukumu lao la msingi kumfikishia mteja mzigo haraka hata kama utakuwa subjected kwenye kodi
 
Hii si kupakana matope ni ukweli usio na chembe ya uzushi na nimeandika kutokana na maudhi ya mfululizo kutoka DHL pamoja na my colleagues ambao pia ni waathirika
 
Mkuu kumbe bado unatumia hawa jamaa. Hawa ni TRA-2 na infact wanafanya kai nyingi kuisaidia TRA kukusanya kodi kuliko kumsaidia mteja kupata migo haraka. Wamekuwa brain washed na TRA
 
Mkuu kumbe bado unatumia hawa jamaa. Hawa ni TRA-2 na infact wanafanya kai nyingi kuisaidia TRA kukusanya kodi kuliko kumsaidia mteja kupata migo haraka. Wamekuwa brain washed na TRA

Kwanza nianze kwa kusema kuwa wakala wa TRA is not a crime maana kodi lazima zilipwe ila jambo la msingi iwe ni Express kama mteja alivyodhamiria.

Ninakubaliana nanyi yaani wewe na mtoa mada, DHL ya hovyo kuliko courier yoyote hapa Tanzania. Mimi niliwahi agiziwa mzigo toka South Africa cha ajabu mzigo ulipokelewa Joberg na within three hours ulikuwa Cape Town na within twelve hours ulikuwa Dar Es Salaam na nilitakiwa niupokelee Mbeya, guess what! ilichukua almost two week kutoka Dar Es Salaam kufika Mbeya toka hapo nikaachana na DHL I go for EMS

DHL ni sheeeeda
 
Nahisi harufu yawakwepa kodi hapa! Hivi mnataka mzigo ukifika hapa usilipiwe kodi? Mkiulizwa hata TIN number zenu mnakuwa wagumu kuwapatia! sasa wataclear vipi mizigo yenu?

Sina intrest yoyote na hawa wajerumani ila mimi nimelipia mzigio wangu Ali express tarehe 7/3/2015 na jana umefika mwanza asubuhi bila shida simply kuwapa full details!

Tusipakane matope kwa uzembe wetu na tulipe kodi! Period
 
the problem its not DHL its DHL custom (TRA section), hawa jamaa wapuuzi kweli kuanzia mkurugenzi wao msukuma yule.
 
Hii si kupakana matope ni ukweli usio na chembe ya uzushi na nimeandika kutokana na maudhi ya mfululizo kutoka DHL pamoja na my colleagues ambao pia ni waathirika
Ni kweli
Ila jitahidi kuandika kwa kifupi
Duh! Gazeti?
 
Hata mimi yamenikuta.Niliagiza mzigo kutoka Aliexpress umefika DHL Dar tangu tar 29 March mpaka sasa unafanyiwa Customs clearance.Sina nia ya kukwepa kodi waniambie nilipie kodi ili nipate mzigo wangu mapema.Sasa kukaa na kitu muda mrefu kwenye clearance kunasababisha hata watu wasiwe na hamu ya kulipa kodi.
 
Kila mtu mwenye nia njema na nchi hii lazima alipe KODI.
Lakini DHL ni courier wa ajabu sana,maana nowdays kila kitu kipo slow kisa TRA,wanaokusanya kodi waangalie na vitu vyenyewe la sivyo itakuwa ni kukera watu na kuona kulipa kodi ni ujanja ujanja.
Nchii hii ina pesa nyingi sana,badala ya kuangaika na kodi za saa nk wakachukue pesa toka kwa hao akina LUGUMI walijitotea pesa kilaini sana!!


 
nataka kusafirisha kifurushi kwenda durban nilitaka kutumia DHL japo mmenitisha! hivi FEDEX bado wapo?
 
Wajanja walikuwa wanaitumia kusafilishia bwimbwi daah watu wabaya...
 
Hii si kupakana matope ni ukweli usio na chembe ya uzushi na nimeandika kutokana na maudhi ya mfululizo kutoka DHL pamoja na my colleagues ambao pia ni waathirika
Acha kupaka matope mkuu, anayesumbua sio DHL bali ni TRA. Kila port of entry kuna afisa wa TRA, sema ishu inategemea afisa wa TRA ni mwadilifu kiasi gani.
 
Acha ukwepa kodi, kila kilichonunuliwa nje ya nchi kinapaswa kulipiwa VAT hata kama ni kalamu. Tatizo la pale DHL sio wao DHL bali ni custom section ambayo ipo chini ya TRA, wala hao DHL hawahusiki bali ni ww mteja na TRA
Ni vyema ukatambua kuwa kazi ya DHL ni shiping tu kama zilivyo shiping lines za kupitia bandari. Kazi ya custom clearance ni ya mteja na TRA. Wewe mteja ukichelewa kumalizana na TRA ndivyo hivyo mzigo wako utachelewa kuwa cleared na ndivyo utavochelewa kuchukua. Kijana lipa kodi acha ujanja ujanja.
 
Unamfundisha samaki kuogelea?
 
Ups nayo imevamiwa. Mzigo wangu tangu tarehe 3 wanacheka cheka nao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…