๐ƒ๐ก๐š๐ซ๐š๐ฎ Z๐š๐ค๐จ Z๐ข๐ญ๐š๐ค๐ฎ๐ฉ๐จ๐ง๐ณ๐š S๐ข๐ค๐ฎ M๐จ๐ฃ๐š

๐ƒ๐ก๐š๐ซ๐š๐ฎ Z๐š๐ค๐จ Z๐ข๐ญ๐š๐ค๐ฎ๐ฉ๐จ๐ง๐ณ๐š S๐ข๐ค๐ฎ M๐จ๐ฃ๐š

wakwatito

Member
Joined
Apr 15, 2018
Posts
30
Reaction score
49
Hebu Jifunze kumuheshimu kila mmoja pasipo Kujali umri au Cheo alichonacho kwasababu Unaweza ukahisi umefanikiwa Sana kwenye maisha yako lakini Kumbe bado mno nakwambia hivyo kwasababu hauwezi kufanikiwa katika kila kitu,

๐Œ๐š๐Ÿ๐š๐ง๐ข๐ค๐ข๐จ ๐ฒ๐š mtu huwa yanapimwa kwa namna kuu nne (4)
Moja wapo ni Imani,
Mbili ni Fedha (Mali),
Tatu ni Elimu (Taaluma)
Mwisho kabisa ni Umaarufu (Kujulikana).

Sasa ajabu ni kwamba Unaweza Ukawa na pesa lakini usiwe na Imani ,
Unaweza Ukawa maarufu lakini usiwe na pesa au ukawa na elimu kuuubwa lakini usiwe na pesa ya kutosha kwahiyo Usipotoshwe na Fedha ukidhani ndiyo kipimo pekee Cha mafanikio ya mtu kwasababu kuwa na Afya njema pia nayo ni mafanikio tosha.

Sikiliza nikwambie hata wewe una kila sababu ya kufanikiwa kwenye maisha yako Tena sana tu Sema Tatizo unajidharau na umejisahau Sana.

Hakuna Shaka Tena juu ya Nini MTU anapaswa Kufanya ili afanikiwe kwani Siri imefichuka (Mambo yapo wazi).

๐‡๐š๐ฒ๐š ๐ง๐๐ข๐ฒ๐จ ๐Œ๐š๐ฆ๐›๐จ ๐ค๐ฎ๐ฎ 9 ๐š๐ฆ๐›๐š๐ฒ๐จ ๐ฎ๐ง๐š๐ฉ๐š๐ฌ๐ฐ๐š ๐ค๐ฎ๐ฒ๐š๐Ÿ๐š๐ง๐ฒ๐š ๐ข๐ฅ๐ข ๐ฎ๐Ÿ๐š๐ง๐ข๐ค๐ข๐ฐ๐ž ๐ค๐ฐ๐š ๐ฏ๐ข๐ฐ๐š๐ง๐ ๐จ ๐ฏ๐ข๐ค๐ฎ๐›๐ฐa
1. Lifahamu Kusudi lako.
2. Chagua Jambo Moja (Niche)
3. Tafuta Maarifa/Knowledge.
4. Tafuta Msimamizi/Mentor.
5. Weka Malengo/Lengo.
6. Gharamia malengo yako
7. Tekeleza kwa dhati.
8. Vumilia na Subiria.
9. Fanikiwa zaidi.

Ukifanya Mambo hayo 9 kwa uaminifu kabisa Basi ni wazi mafanikio yatakuwa sehemu ya Maisha yako na Utashangaa. Swali ni je Wewe unataka kufanikiwa katika Nini ? Na lini unataka uwe umefanikiwa ?

๐‡๐š๐ญ๐š ๐ฐ๐ž๐ฐ๐ž ๐”๐ง๐š๐ฐ๐ž๐ณ๐š ๐ค๐ฎ๐Ÿ๐š๐ง๐ข๐ค๐ข๐ฐ๐š ๐‰๐ข๐š๐ฆ๐ข๐ง๐ข.
Bila shaka unaweza ukawa bado Upo njia panda (Dilemma) hujui Nini ufanye na una Hofu (WOGA) umri unazidi kusogea na hujafanya chochote na pengine bado unaishi kwa watu au umeishi nyumba za kupanga kwa muda mrefu na hujajenga hata kijijini kwenu,huna biashara yoyote Ila Una pesa ya kutumia (Starehe) au Unaamka asubuhi ili ulale usiku na pengine Upo upo tu hujielewi kabisa unashinda ukiangalia series au Movie kila siku.

Usiogope kila kitu kitakuwa sawa.

Kwani bado hujachelewa kuamua.

Kumbuka: Mafanikio ni Gharama.
 
Ukimnyeyekea Kila mtu utafeli bosi..

Nyenyekea anakunyenyekea akila zakiwaki malizana nae
 
Ahsante kwa muongozo...
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom