Dhana ya uhaba wa wanaume huwaweka baadhi ya wanawake katika mahusiano magumu

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,267
29,914
Kuna wakati hutokea wanawake wakateswa sana kwenye uhusiano wao wa kindoa au kimapenzi na bado wakaendelea kukaa tu kwenye uhusiano huo. Inafikia hadi mtu anakufa huku akiona kabisa. Watu wengine huiita hali hii kuwa ni ujinga na wengine huita kulogwa au huelezea hali hii kwa njia ambayo haiwapi haki wanawake hao.

Zipo sababu nyingi ambazo zinawafanya wanawake kuendelea kukaa kwenye mahusiano magumu au ndoa ngumu, bila hata kufikiria kuondoka. Sababu nyingine zinaweza kuonekana kama kituko, lakini ndizo zinazowafanya wang’ang’anie uhusiano huo au wafie kwenye uhusiano au ndoa hiyo.

Kuna dhana imejengeke kwa baadhi ya wanawake kwamba wanaume ni wachache au hakuna wanaume wa kuoa. Dhana hii ambayo haina ukweli wowote, imewafanya baadhi ya wanawake kuishi katika mahusiano magumu na wenzi wao wakihofia kutoka au kuachana nao kwa sababu hawatapata mwanaume mwingine. Kuna wanawake wengi sana ambao wanagombea kupendwa, au wanajipendekeza ili wapendwe.

Hawa ni wanawake ambao wana kasoro kubwa kwenye mifumo yao ya kufikiri au ufahamu. Unaweza kukuta mwanamke anadhalilishwa, anaoneshwa kwamba hatakiwi, amechokwa, ameshachezewa lakini amemng’ang’ania mwanaume huyo kama luba.

Wanawake wanaoteswa kwenye uhusiano au ndoa, huwa wanajidanganya kwamba, watamudu siku moja kubadili tabia hiyo a waume zao kuwafuja. Wanajiambia kwamba, kutukanwa, kupigwa, kudhalilishwa, na matendo mengine, kuna siku watamudu kuwasaidia wanaume hao watoke kwenye tabia hizo. Lakini wakati mwingine wanaume hawa watesaji, huwa wanajidai kusema kwamba, wanafanya mambo hayo bila kujua sababu na kuna wakati wanasema wamelogwa.

Hujawahi kuwaona wanawake wanaokwenda kwa waganga kutafuta dawa ili waume zao wasiwapige, ati kwa sababu vipigo vyao vinatokana na kuchanganywa na uchawi wanaofanyiwa na wanawake zao wa nje? Mwanamke anaamini kabisa kwamba, mumewe hamjali na anamdhalilisha kwa sababu ya kulogwa!

Mwanamke anaweza kujiambia kwamba, kwa sababu mume wake kuna wakati anamtendea wema, hata kama ni mara moja, basi anampenda na hayo mengine mabaya, yatakwisha au ni bahati mbaya. Mwanamke pia anaweza kufikiri kwamba, akijitahidi sana kumfurahisha mumewe, mume huyo atabadilka na kuwa na tabia nzuri.

Hivyo hujipendekeza na mwanaume habadiliki na mateso yanaongezeka. Kuna wanaomudu kutoka kwenye uhusiano wa aina hiyo, hawa ni wale ambao wanajua nini maana ya kupenda wao hawasukumwi na mihemko, bali husukumwa na kupenda.

Kwao msamiati kwamba wanaume ni wachache au hakuna wanaume wa kuoa haupo kabisa akilini mwao..............    
 
yaani kung'ang'ania kwa mwanaume anayetea, anayepiga, anayefuja ni upumbavu ulofa na ujinga........... bahati mbaya ujinga huu umewajaa badhi ya wanawake....tena wanashauriana kuvumilia "wanaume" ndivyo walivyo,

ni ujinga na upumbavu

na kutokujiamini

(ingawa na malezi pia yanachangia)
 
Ukweli ubaki kuwa ukweli, wanaume tupo wachache siku hizi. Ila kwenye suala la mwanamke kudhalilishwa daily halafu bado kang'ang'ana tu huo ni utumwa.
 
yaani kung'ang'ania kwa mwanaume anayetea, anayepiga, anayefuja ni upumbavu ulofa na ujinga........... bahati mbaya ujinga huu umewajaa badhi ya wanawake....tena wanashauriana kuvumilia "wanaume" ndivyo walivyo,

ni ujinga na upumbavu

na kutokujiamini

(ingawa na malezi pia yanachangia)
Nyie ni Ving'ang'aniz sana a thee

Mtu Anaweza kupigwa mpaka akazimia zen kesho anaambiwa I love u Na yeye anasema Love u too
 
pia kutojitambua kunachangia aisee...

kuna wanawake wanapigwa hatari ila wapo tu

kuna wengine hata wakifiwa na wazazi hawaendi kuzika ila wamo tu

kuna wengine wanatukaniwa mpaka bibi na babu zao waliopo kaburini ila wapo tu

kuna wengine wanaume chupi mkononi suruali magotini lakini wenyewe wameng'ang'ana tu......

wanawake wa namna hiyo ni malofa...... pia malezi yanachangia, kama kakua akiona mmoja wa wazazi wake ananyanyaswa inamjenga akilini kuwa kunyanyaswa ndoani ni kitu cha kawaida.

inabidi wajitambue thamani zao......

kwa nini binadamu mlokutana na meno 32 akunyasenyase?(akunyanyase)


Nyie ni Ving'ang'aniz sana a thee

Mtu Anaweza kupigwa mpaka akazimia zen kesho anaambiwa I love u Na yeye anasema Love u too
 
Muda mwingine hii yote inasababishwa na baadhi ya wanawake kuwa tegemezi ndio mana akili zime lemaa na kujua hakuna maisha mengine bila huyo mume kumbe maisha popote.

Hili somo zuri ila ni gumu kuingia kwa baadhi ya vichwa vya wanawake wenzangu kwani kuna wengine wakipenda hata wafanyiwe maudhi ya aina gani wao kwao wanaona wanapendwa.
 
Muda mwingine hii yote inasababishwa na baadhi ya wanawake kuwa tegemezi ndio mana akili zime lemaa na kujua hakuna maisha mengine bila huyo mume kumbe maisha popote.

Hili somo zuri ila ni gumu kuingia kwa baadhi ya vichwa vya wanawake wenzangu kwani kuna wengine wakipenda hata wafanyiwe maudhi ya aina gani wao kwao wanaona wanapendwa.
Utegemezi nao unachangia......
 
Back
Top Bottom