Dhana ya Kudai Demokrasia Ianzie kwenye VYama Vyetu Kuakisi madaraka makubwa tunayotaka kwenye nchi

mayaJr45

JF-Expert Member
May 12, 2016
560
205
Siasa ya tanzania kila leo imejikita kwa asilimia kubwa kudai demokrasia na utawala wa sheria katika dola.Nimuelekeo mzuri sana hasa pale unapokua haujapata kushika hiyo dola .

Nimeamua kuandika hivi kwa maana kubwa siasa za nchi ya za Africa kwa zaidi ya asilimia tisini zinafanana.Mfano tumetoka kuona Comredi Robert Mugabe,Kagame ,Kabila,Nkurunzinza wakiwa mifano kwa utashi tofauti wa jambo hili.Ukifuatilia historia ya watu hawa utakuja na majibu mbalimbali tofauti ila mwisho wa siku jibu kubwa na la msingi ni ngumu kuachia madaraka ukiwa nayo tayari.

Leo najikita kwenye jambo hili nikilishusha kwenye vyama vyetu vya siasa .Tumeshasikia misuguano mbalimbali NCCR MAGEUZI toka enzi za kina Mabere Marando ,Lamwai na MREMA,CUf Hamadi Rashidi na maalim seif ,CHADEMA Zitto kabwe na mh mbowe .Kimsingi ukifuatilia mambo haya unakuta ni kukosa Demokrasia kunogewa na madaraka na kuona kanakwamba bila watu flan au nila mimi chama flan sio chama .

Hauwezi kuwa mpigania demokrasia wakati wewe kwenye taasisi yako ambayo ni daraja lako umeshindwa kuweka misingi ya kuheshimu katiba na demokrasia .Mwanzo kuna kuwa na mipango mingi urais mwisho miaka kumi ,uenyekiti wa chama mwisho miaka 10 ukiona miaka kumi inafika mtu hataki kuondoka anaweka misingi na mikakati mipya ya yeye kuendelea kuwepo huyo si mfuasi wa demokrasia katika level yeyote yakichama wala katika taifa.

Mwisho namaliza kwa kusema angalau kwa asilimia flan tujenge dhana na picha flan ndogo kwenye vyama vyetu inayo akisi picha kubwa ya madaraka ambayo tunapigania kwenye nchi.
 
Back
Top Bottom