Mpita Njia
Platinum Member
- Mar 3, 2008
- 6,999
- 1,189
Wapi Ritz?
Nalo neno mkuu.Dhamira yangu kama mwananchi ni kuona watanzania wengi wanaamka na kuanza kuchapa kazi na kushiriki katika shughuli mbalimbali za uchumi na uwekezaji. Kuangalia timu za hispania naangalia kwa luninga yangu if I have time
hilo la kutembelea mbuga linanifanya nihisi kuna jambo hapa!waletwe kwa cost zetu na mbugani wapelekwe bure!ngachoka kuchuRais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa bado
ni dhamira ya Serikali yake kuileta moja ya timu za Ligi Kuu ya Soka ya
Hispania La Liga kutembelea Tanzania na amemtaka Balozi mpya wa
Hispania katika Tanzania kusaidia kufanikisha dhamira hiyo.Aidha, Rais
Kikwete ameipongeza Hispania kwa kufanikiwa kutetea Ubingwa wa Kombe la
Mataifa ya Ulaya katika mashindano yaliyomalizika mwezi uliopita katika
Poland na Ukraine.Akizungumza na Balozi mpya wa Hispania, Mheshimiwa
Luis Manuel Cuesta Civis mara baada ya kupokea hati yake ya utambulisho
katika hafla fupi iliyofanyika leo, Alhamisi, Agosti 16, 2012, Ikulu,
Dar es Salaam, Rais amesema:Wananchi wa Tanzania, ambako timu za
Hispania, zina washabiki na wafuasi wengi, bado wanasubiri kwa hamu
ziara ya moja ya timu kubwa za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania. Tunataka
ije hapa, icheze mechi moja ama mbili na itembelee mbunga zetu maarufu
za wanyama, amesema Rais Kikwete na kuongeza:Kama utakavyokuja
kuthibitisha mwenyewe, Watanzania ni watu wanaopenda michezo na hasa
soka na ni wafuatiliaji wakubwa wa Ligi Kuu ya Hispania ambako timu
zenye mvuto zaidi ni Real Madrid na Barcelona.Rais Kikwete pia
ameipongeza Hispania kwa kutetea ubingwa wake wa Kombe la Mataifa ya
Ulaya katika mashindano ya Euro 2012 yaliyomalizika karibuni katika
Poland na Ukraine.Tunawapongeza sana kwa kuweka historia. Kwanza
mlishinda Kombe la Mataifa ya Ulaya, kisha mkashinda Kombe la Dunia.
Sasa mmeweza kutetea Kombe la Ulaya. Hili halijapata kutokea kwa nchi
moja kushikilia vikombe vyote viwili vikubwa vya soka duniani kwa wakati
mmoja ama nchi kutetea Kombe la Ulaya.EndsNOTE: Taarifa hii imetumwa
na salva kwa vyombo vya habari jioni hii
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa bado ni dhamira ya Serikali yake kuileta moja ya timu za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania La Liga kutembelea Tanzania na amemtaka Balozi mpya wa Hispania katika Tanzania kusaidia kufanikisha dhamira hiyo.Aidha, Rais Kikwete ameipongeza Hispania kwa kufanikiwa kutetea Ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya katika mashindano yaliyomalizika mwezi uliopita katika Poland na Ukraine.Akizungumza na Balozi mpya wa Hispania, Mheshimiwa Luis Manuel Cuesta Civis mara baada ya kupokea hati yake ya utambulisho katika hafla fupi iliyofanyika leo, Alhamisi, Agosti 16, 2012, Ikulu, Dar es Salaam, Rais amesema:Wananchi wa Tanzania, ambako timu za Hispania, zina washabiki na wafuasi wengi, bado wanasubiri kwa hamu ziara ya moja ya timu kubwa za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania. Tunataka ije hapa, icheze mechi moja ama mbili na itembelee mbunga zetu maarufu za wanyama, amesema Rais Kikwete na kuongeza:Kama utakavyokuja kuthibitisha mwenyewe, Watanzania ni watu wanaopenda michezo na hasa soka na ni wafuatiliaji wakubwa wa Ligi Kuu ya Hispania ambako timu zenye mvuto zaidi ni Real Madrid na Barcelona.Rais Kikwete pia ameipongeza Hispania kwa kutetea ubingwa wake wa Kombe la Mataifa ya Ulaya katika mashindano ya Euro 2012 yaliyomalizika karibuni katika Poland na Ukraine.Tunawapongeza sana kwa kuweka historia. Kwanza mlishinda Kombe la Mataifa ya Ulaya, kisha mkashinda Kombe la Dunia. Sasa mmeweza kutetea Kombe la Ulaya. Hili halijapata kutokea kwa nchi moja kushikilia vikombe vyote viwili vikubwa vya soka duniani kwa wakati mmoja ama nchi kutetea Kombe la Ulaya.EndsNOTE: Taarifa hii imetumwa na salva kwa vyombo vya habari jioni hii