Dhahabu ilivyo wakutanisha Ma-DC, Kiteto na Kilindi porini

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
449
60
Tanzania imetajwa kuwa na madini ya kila aina, madini hayo yametajwa kuwa ya thamani kubwa hali inayofanya wengi wao kujihusisha na kazi hiyo.

Serikali kwa kuona hayo imekuwa karibu na wananchi kwa kufuatilia nyendo na taratibu zao katika kazi hiyo.

Madini ya dhahabu yanayochimbwa mlima wa Mangedwa wilaya ya Kilindi mpakani mwa Kiteto karibu na Kijiji cha Mesera na kitongoji cha Kwasakala, Tarafa ya Kwakivu wilayani Kilindi yamekutanisha wakuu wa Wilaya hizo kushuhudia uchimbaji huo.

Zaidi ya watu 300 wakiwemo akinamama wamevamia mlima huo na kuanza shughuli za uchimbaji wa dhahabu hiyo, huku wakiwa hawana vifaa vya kitaalamu, huduma za jamii kama vile maji, afya, vyoo, maduka na hata migahawa kuwezesha shughuli hiyo.

Wakiwa katika eneo hilo wakuu hao wa Wilaya wametambua shughuli hiyo kwa kuwataka wachimbaji hao kufanya kazi hiyo kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhandisi Tumaini Magessa akizungumza hayo alisema Serikali inatamani kuona kila mwananchi akifanya kazi halali na kuwataka wachimbaji hao kujali afya zao kwa kuanza kuwa na matundu ya vyoo.

Pia aliwataka wawe na elimu ya uchimbaji wa madini hayo kwa kutumia wataalamu waliopo wilayani kuepuka hasara kwa kufanya kazi hiyo kienyeji bila tija

Alisema baada ya kupata taarifa ya watu hao kuwa katika eneo hilo bila kujali eneo walio aliwasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi ili kutaka waanze kupata huduma japo kuwapa elimu ya usafi, katika uchimbaji wa madini nk

Mkuu wa Wilaya ya Kilindi aliwataka wachimbaji hao kufanya kazi kwa tija huku akiwahakikishia kuwa Wilaya imejipanga kuwa na maduka ya kununua madini kama maelekezo ya Rais Magufuli yalivyo.

Mamia ya wananchi hao wamezagaa katika mlima huo wakiendelea na shughuli za uchimbajibhuo wa Dhahabu huku kukiwa hakuna huduma muhimu ambapo Serikali ameahidi kutoa ushirikiano kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona wanalima na Alizeti japo kwa uchache, lakini mahindi na maharage ndio kwa wingi. Wenyeji wanakwambia msimu wa hayo mazao kuna pesa balaa, lakini hakuna maendeleo yoyote yale siju ndio ushirikina.
Kuna zao gan la biashara zaidi ya maharagr mkuu?
 
Naona wanalima na Alizeti japo kwa uchache, lakini mahindi na maharage ndio kwa wingi. Wenyeji wanakwambia msimu wa hayo mazao kuna pesa balaa, lakini hakuna maendeleo yoyote yale siju ndio ushirikina.


Kuna mate naye analima huko miaka zaidi 10...lakini sijaona km ananuru!
 
Naona wanalima na Alizeti japo kwa uchache, lakini mahindi na maharage ndio kwa wingi. Wenyeji wanakwambia msimu wa hayo mazao kuna pesa balaa, lakini hakuna maendeleo yoyote yale siju ndio ushirikina.

Hivi maharage ya huko na ya Ngara yapi mazuri mkuu? Naona maharage huku mazuri sana yana ladha! Sema naona yako juu..2700@kg
 
Back
Top Bottom