LEO KATIKA UCHUMI
Deni la taifa ni nini? (National Debt)
Deni la taifa ni pesa taslimu au rasilimali iliyokopwa na serikali kutoka kwa mashirika ,makampuni mabenki, taasisi au watu binafsi ndani ama nje ya nchi ili kuziba nakisi ya bajeti yake Karina kutekeleza miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida.
Kwa nini linaitwa deni la taifa na si deni la serikali? Ni deni la taifa kwani serikali hukopa ili kuhudumia raia wote bila ubaguzi na wajibu wa kulilipa upo kwa raia wote kupitia kodi wanazolipa kwa serikali.
Yapi matumizi sahihi serikali inapokopa fedha?
Ni sahihi sana serikali inapokopa ili kutekeleza miradi ya maendeleo (development expenditures) kama ujenzi wa barabara, viwanda, ununuzi wa meli na ndege za abiria na mengine mengi yanayoendana na haya. Kwa nini matumizi haya ni sahihi? Kwa sababu kama miradi hii ikitelezwa kwa weredi na kwa ubora stahiki inaweza kulipa deni pasipo kuwaumiza wananchi kwa kuwatoza kodi kubwa ili kulipa deni hilo. Lakini pia miradi hii ni vichochezi vya kukuza uchumi katika maeneo mbalimbali miradi hii inamotekelezwa. Hii hupanua wigo wa kodi (widen the tax base) yaani huweza kuongeza makusanyo ya kodi kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi(multiplier effects of investments). Serikali hapa hujipa uweza wa kupanga na kutekeleza mipango yake vizuri.
Ni nini matumizi yasiyofaa kwa pesa ya mkopo?
Serikali inapotumia pesa iliyokopa kulipa mishahara na poshoza watumishi ,kununulia madawa ya hospitali, kufanya uchaguzi wa viongozi na yaendanayo na haya si vibaya sana lakini uwezekano wa serikali kulipa madeni haya huwa mdogo kwani shughuli hizi hazizalishi kipato. Mbaya zaidi huwa pale serikali inapotumia pesa iliyokopa kununulia silaha za kijeshi na kufanikisha vita ambayo huwa haina faida kwa raia kabisa. Matumizi yote niliyotaja katika aya hii hufanya mkopo huu wa serikali uitwe MKOPO ULIOKUFA( DEAD WEIGHT LOAN).Ni mkopo uliokufa kwa sababu umeelekezwa kwenye matumizi yasoyozalisha hivo kulipwa kwake kutatokana na vyanzo tofauti vya mapato vya serikali hasa kodi.
Raia anaumizwa vipi na matumizi mabaya ya mikopo ya serikali?
Moja, raia atatozwa kodi kubwa ili serikali ilipe deni kutokana na mashinikizo makubwa kutoka mataifa na taasisi kubwa duniani ikiwemo kushikilia mali za serikali zilizo nje ya nchi kma meli za Argentine zilipozuiwa miezi kadhaa iliyopita.
Pili raia huweza kuishi maisha magumu sana ikiwemo kupata huduma duni za kijamii kma elimu, afya, maji na nyinginezo wakati serikali ikiwa inatumia rasilimali zake kulipa deni ambalo halikuzaa matunda bora kwa raia.
Tatu, raia huweza kulipa Deni ambalo hakufaidi matunda yake. Kwa mfano, mtu aliyezaliwa mwaka 1990 sasa hivi ni mtumishi au mjasiliamali na analipa kodi .Iwapo kodi hii inatumika kulipa deni lasilaha za kivita ya Vita ya Kagera dhidi ya Idd Amin ya mwaka 1978/79 huyu anaumizwa kwa kitu kisichomhusu. Hivo busara inahitajika ktk kukopa na kutumia.
Nani ana wajibu kuwalinda wananchi ktk hili?
Wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi ndio wenye wajibu wa kuisimamia serikali na kuhakikisha matumizi yote yanamnufaisha raia.Wabunge hawapaswi kutuambia serikali haisikii angali katiba imewapa ruksa kuiwajibisha serikali bila kujali tofauti za vyama vyao. Ukiona mbunge ulompa kura anarudi kujitetea kuwa serikali haisikii jua hajui nguvu zake kikatiba na hana nguvu ya ushawishi na weredi ili kuwaelimisha wenzie kufikia maamuzi sahihi.
Tujielimishe ili tuwe wapiga kura wazuri na raia bora na wawakilishi bora wa kizazi kijacho.
Sent using Jamii Forums mobile app