Kwa utaratibu huu wa demokrasia yangu,kungekuwa na vituo vingi vya kutolea maoni kote nchini kadri tume itakavyoona inafaa.Kila kituo kingewahusisha idadi maalum ya raia.
Kituo kama hicho kingekuwa na akaunti yake NEC.Maoni ambayo yangepewa nafasi ni yale tu yatakayopitia akaunti hizi pekee.
Kwa demokrasia hii,mgombea mwenye tatizo lolote lenye kuvunja heshima ya kuwa kiongozi hawezi kufikia kiwango cha kupata umaarufu kwani matatizo yake yatajulikana mapema.
Namna nyengine ambavyo demokrasia hii inafanya kazi ni kuwa mtu ambaye yuko madarakani,iwapo vituo vingi vitaonesha kutoridhishwa naye kwa jinsi ambavyo ataoneshwa kasoro zake na tume ikaridhika na tuhuma hizo, basi ataondoka madarakani mapema bila gharama yoyote.