Demokrasia imeleta dhiki na ghasia duniani huku waathirika wakubwa ni wakereketwa

mbegubora29

JF-Expert Member
Mar 14, 2015
483
294
Fanya ufanyavyo mfumo wa kidemokrasia hauwezi kuwakomboa wananchi kutokana na shida walizonazo. Kwanini siuamini? Huu mfumo nimejarbu kuutumia katika familia yangu sijafaulu.

Yaani iko hivi Mimi ndo baba niliruhusu demokrasia katka chakula cha usiku ila niliishia kuchanganyikiwa mwisho nikatoa maamuzi kama baba basi pakaliwa,

NB: Ila tofauti yangu sikuikemea wala kuitukana familia yangu, sijaiteka na hata wale ambao hawakuridhika niliwafariji na wote baada ya kushiba walinielewa ila maendeleo kwa kile nilichojaaliwa nawahudumia!
 
Na wanasiasa wanaotudanganya tuandamane wao wana visa mkononi za Nchi za mabeberu

Kikinuka tu wanabeba family zao watatuacha sisi tuvurugane
 
Binaadamu tunachofeli ni kupambana na nafsi zetu, nafsi "ikipenda/ikichukia/ikitaka" "kitu/mtu/jambo" basi mengine hua hatujali kabisa, hatujali haki imetendeka au haijatendeka, hatujali hisia za wengine, hatujali madhara ya maamuzi yetu, hatujali hicho kitu umuhimu wake, hatujali chochote. Kila binaadamu ana chembe chembe za roho mbaya, hakuna binaadamu asie na roho mbaya (Every soul is biased to some extents and has selfish elements & motives).

Tunachojali ni "NAFSI" zetu ziridhike tu, na kama mtu akiweza yeye binafsi kupambana na nafsi yake vilivyo, basi wanaomzunguka hawataweza kupambana na nafsi zao. Hivyo lazima tatizo liwepo tu.

Demokrasia bila kutenda "HAKI/KUPAMBANA NA NAFSI" lazima tafrani liwepo. Halikwepeki.

MFANO MZURI: Wewe na familia yako, wewe binafsi uliweza kupambana na nafsi yako na kutoa uhuru katika familia yako kwenye chakula cha usiku, kwa hilo uliweza kutojali nafsi yako inachopenda, ila wanafamilia hawakuweza kupambana na nafsi zao kama wewe ulivyoweza.
 
Back
Top Bottom