Ded Kiteto awa Mbogo

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Naam kwa uwezo wa Mungu tena nakutanishwa nanyi katika mengi yahusuyo Nchi yetu

Kwa Kiteto pamoja na mambo mengine, Mkurugenzi mtendaji wa halm ya Wilaya ya Kiteo Tamim Kambona ametoa onyo kwa wazazi na walezi ambao watawakatisha watoto wao masomo kwa kuwaozesha ama kuchunga mifugo.

Hatua hiyo imetokana na idadi kubwa ya wanafunzi kukatishwa masomo huku baadhi ya wananchi wakiwa vinara katika zoezi hill

Amepongeza Shule ya msingi Lalakir iliyopo kata ya Partimbo kwa kuongoza mara kadhaa katika mitihani ya Taifa

Shule ya msingi Lalakir imekuwa ya kwanza kila mwaka Kiwilaya na mwaka Jana ilikuwa ya tatu Kimkoa na kitaifa ya 53

Ufaulu huu umekonga nyoyo za wadau mbalimbali wa elimu na kuapa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha elimu shuleni hapo.

Hats hivyo wanafunzi waliohitimu darasa la saba wameapa kuendelea kulinda nafasi yao hiyo Kitaifa pamoja na kwamba wasimamizi wa mitihani kila mwaka hutoka Taifa katika Shule hiyo.

Mkurugenzi Kambona aliwaahidi waalimu hao kuwapeleka mbuga za wanyama hapa nchini kama Zawadi kwao kwa kufaulisha kwa kiwango cha juu

Mbali na hilo pia ameahidi kujenga majengo mbalimbali shuleni hapo ili kuendeleza jitihada za walimu na wanafunzi katika elimu.
 

Attachments

  • DSCF7128.JPG
    42.6 KB · Views: 27
Picha iko tofauti na umbogo, vipi na yeye atasukuma ndani?
 
Asante kwa picha mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…