Sikubaliani na BAKITA wanaposema mfumo wa dijitali uwa mfumo wa dijiti au wa kidijiti.
Kwa maoni yangu uwe MFUMO WA TARAKIMU kwa vile digit = tarakimu.
Sikubaliani na BAKITA wanaposema mfumo wa dijitali uwa mfumo wa dijiti au wa kidijiti.
Kwa maoni yangu uwe MFUMO WA TARAKIMU kwa vile digit = tarakimu.
Kwa mujibu wa mjadala ulioendeshwa kupitia radio 1 katika kipindi cha ulimwengu wa kiswahili, kinachurushwa kuanzia saa 1:30 asubuhi (MUHIMU: kipindi kilirushwa siku ya jumamosi ya tarehe 5/1/2013); DECODER = KISIMBUZI na DETECTOR = KING'AMUZI.
Decode ni muunganiko wa maneno mawili, CODE na DE, na neno DE limetumika kama kikanushi/kinyume. Mfano: KWELI na SI KWELI. CODE linatafsirika kama SIMBA (sio simba mnyama) kwa lugha ya kiswahili. Na DECODE linatafsirika kama SIMBUA wa lugha ya kiswahili. SIMBA (sio simba mnyama) kinyume chake ni SIMBUA. Na kifaa kinachotumika kusimbua kinaitwa KISIMBUZI, yaani DECODER kwa kingereza.
Lakini neno DETECTOR tafsiri yake ni KING'AMUZI. Na ving'amuzi viko vya aina nyingi, mfano:
Metal, X-rays, Uranium, Gas, Moisture, Blood sugar na Bomb DETECTORS; yaani ving'amuzi vya kung'amua metali, miale ya X, madini ya Uranium, Gesi, Unyevu, sukari ya damu na mabomu.
Kumbuka DECODER = KISIMBUZI na DETECTOR = KING'AMUZI.