Dear Atheists, this thread’s for you — Everyone else, keep scrolling!

Hoja nzuri sana hii.
 
Una elewa maana ya uhakika?

Unataka uhakika na uthibitisho upi kwa kisichokuwepo?

Kukuta watu wanasema kuna Mungu, Hakufanyi Mungu huyo awepo.

Tumezaliwa na kukuta kuna watu wanasema kuna Dragons watemao moto midomoni mwao, Lakini kiuhalisia hawapo.

Sawa na wewe, umezaliwa na kukuta watu wanasema kuna Mungu, Na wewe ukaunga msafara kuendeleza kusema hivyohivyo, Kuna Mungu! Kuna Mungu! Kuna Mungu!

Lakini kiuhalisia Mungu huyo hayupo.

Mungu ni sawa na Abunuwasi wote wana exist kwenye vitabu tu. Sio kwenye uhalisia.

Mungu ana exist kwenye hekaya za Biblia, Quran, Torah n.k

Abunuwasi ana exist kwenye hekaya zake za vitabuni.

Unarithishwa kitu bila hata kukifanyia uchunguzi wake.
 
Usiseme mimi nimezaliwa na kukuta watu wanasema kuna Mungu bali wote tumezaliwa na kukuta watu wanasema hakuna Mungu na wengine wanasema Mungu yupo, na watu wamekuwa wakibadili misimamo katika hiyo mitazamo miwili ya kudai Mungu yupo/Mungu hayupo yani unaweza kumkuta mtu leo anasema Mungu hakuna na kesho anabadili na kusema Mungu yupo au mtu kalelewa katika kuamini Mungu yupo ila baadaye anabadili na kufuata mtazamo wa kudai Mungu hayupo.

Sasa katika mazingira kama hayo wewe utasemaje una uhakika hakuna Mungu? kwa sababu kama kweli nyinyi mnaodai hakuna Mungu mna uhakika bila shaka sasa inakuaje tunaona baadhi ya waliyo kuwa wenzenu(wanasema hakuna Mungu) waliachana madai hayo yenye uhakika na kwenda kuamini Mungu kusiko na uhakika? Hii inawezekanaje? Ndio maana nauliza huo uhakika uliyonao wewe ni upi?

Kama unadhani kutokuwa na uthibitisho wa kuwepo Mungu ndio unatumia kusema kwamba et una uhakika hakuna Mungu basi upo wrong.

Halafu kuna watu hata hawaamini vitabu vya dini ila wanakubali uwepo wa Mungu/miungu, hivyo usikariri.
 
Hivi kitu kimoja kinaweza kikawepo na kisiwepo kwa wakati mmoja?

Ni either kitu kipo au hakipo.

Mungu hayupo.

Ukibisha thibitisha yupo.

Usianze stori hapa na unnecessary explanations.
 
Mungu aliumba dunia isiyokuwa na maovu. Uovu ulianza baada ya wanadamu wa kwanza kuasi agizo la Mungu.
Mwanzo 1:31
Mungu akaona kila kitu alichokiumba ni chema kabisa.
Aliiumba dunia akiwa tayari keshamtimua shetani(kwa mujibu wa script yenu ya biblia) huko mbinguni?
 
Acha uongo, Musa hakuuona uso wa Mungu ila aliona sehemu ya nyuma kwa mujibu wa kitabu chenu na alizimia, hakufa. Acha uongo
 
Hivi kitu kimoja kinaweza kikawepo na kisiwepo kwa wakati mmoja?

Ni either kitu kipo au hakipo.

Mungu hayupo.

Ukibisha thibitisha yupo.

Usianze stori hapa na unnecessary explanations.
Kwanini wewe utoe madai kwa maneno matupu tu unasema Mungu hayupo na unataka wote tukubali kuwa huo ndio ukweli halafu et kama tutataka kukubishia basi tunatakiwa kuthibitisha kuwa yupo?

Unachofanya ni sawa kabisa na kusema tu kwamba chumba anacholala Rais Samia hakuna Tv ya flat screen na kwamba tukibisha basi tuthibitishe kuwa ipo hiyo tv ya flat screen.

Yani unatakiwa uelewe kwamba huwezi kukaa na kujiamulia kusema tu kwamba kitu fulani hakipo, lazima utaulizwa umejuaje? Ni kweli kitu hakiwezi kuwepo na hapo hapo kikawa hakipo, kusema kuwa kipo au hakipo kuna hitaji kujua sasa tatizo wewe hauelezi umejuaje kiuhakika kuwa Mungu hayupo?

Nimeeleza kwamba watu wamekuwa wakihama hama huyu anasema Mungu yupo kesho anasema hayupo na yule anasema Mungu hayupo na kesho anasema yupo. Sasa kama wewe unajua kiuhakika usio na shaka kuwa Mungu hayupo kwanini usieleze hapa ili wote tujue ukweli?
 
HAYA MAMBO HAYA AU BASI
 
Mimi napinga madai yenu ya kwamba kuna Mungu.

Toeni uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu.

Unless otherwise huyo Mungu hayupo.

Kama huelewi basi.

Acha kukaza fuvu na kuleta unnecessary explanations zisizo na logic.
 
Mimi napinga madai yenu ya kwamba kuna Mungu.

Toeni uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu.

Unless otherwise huyo Mungu hayupo.

Kama huelewi basi.

Acha kukaza fuvu na kuleta unnecessary explanations zisizo na logic.
Wewe ndio huelewi na ndio najaribu kukuelewesha uelewe unachokisimamia, kama unapinga madai yetu ya kusema kuna Mungu na kupinga huko kama ni kwa sababu hatuna uthibitisho basi wewe usingekuwa unasema tena kwa uhakika kuwa hakuna Mungu kitu kinachoonyesha kwamba unajua kabisa hakuna Mungu na si kwamba unapinga tu madai ya kuwepo kwa Mungu kwa kukosekana uthibitisho.

Kwa sababu ya upungufu wa uelewa wako ndio maana unashindwa kujua kwamba unachofanya wewe ni kutoa madai kwamba unajua hakuna Mungu, na kwamba kama kuna mtu anakubishia basi atoe uthibitisho wa kuwepo Mungu ili ku prove wrong madai yako wewe ndio unachokufanya hapa.

Najua atheists hamjazowea challenge kwenye huo msimamo wenu maana huwa mnaamini kwamba mpo sahihi tu moja kwa moja hivyo kazi yenu ni kushambulia imani ya Mungu na kudai uthibitisho basi ndio maana hapa unaona naongea vitu visivyoeleweka.

Huwezi ukasema unapinga madai ya kuwepo Mungu kwa sababu hakuna uthibitisho wakati teyari mwenyewe unadai kwa uhakika kuwa Mungu hayupo na ndio maana kukosekana kwa uthibitisho wa kuwepo Mungu mnakutafsiri ni kama ku prove madai yenu ya kwamba hakuna Mungu.
 
I rest my case with you.

Huelewi hata falsafa ya uthibitisho inamtaka yule anayedai kitu kipo ndio atoe uthibitisho wa hicho kitu.

Wewe unataka upewe uthibitisho kwa kitu kisichokuwepo, wakati madai ya kusema kitu hicho kipo ni ya kwako.

Unakataa kwamba hakuna Mungu wakati huwezi kuthibitisha kuna Mungu.

Sasa unataka nini?

You just bring unnecessary explanations.
 
Hakuna hata sehemu moja niliyokwambia uthibitishe tatizo umekariri, mimi nakuuliza wewe umejuaje kiuhakika kuwa Mungu hayupo? Sasa umeulizwa umejuaje kuwa hicho kitu hakipo wewe unasema et umeambiwa uthibitishe kisichokuwepo.

Sema dogo huwezi kunielewa nitakuchosha tu.
 
Unataka mimi nikwambie nilijuaje Mungu hayupo, wakati wewe mwenyewe unayedai yupo hujui yupoje?

Yani unataka nikwambie kisicho kuwepo jinsi ambavyo hakipo. Wakati wewe unayedai kipo, hujui hata kipoje.

You need to restore your brain to factory settings.
 
Tatizo lako hujui kuwa una claim kuwa unajua kwamba Mungu hayupo sasa ukiulizwa umejuaje hujui umejuaje, sasa ikiwa mie sijui hicho nachosema kipo sijui kikoje ndio hapo sasa najiuliza wewe umewezaje kujua kiuhakika kuwa hakipo hicho kitu? Umeenda huko kinadapodaiwa hicho kitu kipo ukakikosa au umejua kwa namna gani hasa?
 
Una elewa maana ya kupinga na kudai?

Mimi sidai Mungu hayupo.

Napinga Mungu yupo.

Kwa hivyo napinga madai yenu.

Madai yenu yanasema "kuna Mungu" Mimi napinga madai yenu kwa kusema hakuna Mungu.

Mimi sina madai yeyote kuhusu Mungu.

Mimi nina pingamizi kuhusu huyo Mungu wenu.

Ninapinga uwepo wa Mungu.

Una elewa kiswahili?
 
A message to all atheists. You are all correct in your own perspective until your end when you meet the best preacher (DEATH). In your last seconds you will realize the truth. Just be persistent with what you believe until then.
 
A message to all atheists. You are all correct in your own perspective until your end when you meet the best preacher (DEATH). In your last seconds you will realize the truth. Just be persistent with what you believe until then.
You are suffering from irrational fear.

You have fear of unknown.

If you believe in God just because of the fear of death. Just know that you are suffering from irrational fear, phobia and extreme anxiety because none of us will escape it.

You need to restore your brain to factory settings.
 
Shida sio kupinga bali ni sababu ya kupinga. Yupo mtu anaweza madai ya uwepo wa Mungu kwa sababu hakuna tu uthibitisho ila si kwamba anajua kiuhakika hakuna Mungu ndio maana anapinga madai ya kuwepo Mungu, ila wewe unapinga madai ya kuwepo Mungu kwa sababu unajua huyo Mungu hayupo ndio maana unapinga madai yenye kusema Mungu yupo.

Huwa unatoa kauli ya madai kwa kusema Mungu hayupo na kama mtu anabisha athibitishe, maana yake umetoa madai ya kwamba Mungu hayupo ila kama mtu atabishia madai yako basi atapaswa kutoa uthibitisho ambao ndio utaku prove wrong madai yako.

Kwahiyo wewe ni kweli unapinga ila unapinga kwa sababu unadai hakuna huyo Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…