DC Waryuba akabidhi vitambulisho vya Harmonize

DC Waryuba akabidhi vitambulisho vya Harmonize

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
Mkuu wa wilaya Tandahimba Mhe. Sebastian Waryuba amekabidhi vitambulisho kwa Wajasiliamali wadogo 50 ambavyo Msanii Harmonize wa kundi la Wasafi aliwanunulia Wajasiliamali hao.

DC Waryuba amekabidhi vitambulisho hivyo nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kumshukuru Msanii Harmonize kwa moyo wake wa upendo kwa Wajasiliamali wadogo na kumuunga mkono Rais Magufuli ambaye ndiye aliyetoa Vitambulisho hivyo.

"Sisi wana Tandahimba tunamshukuru sana Msanii Harmonize kwa kutimiza ahadi yake ya msaada wa vitambulisho 50 alivyotoa kwa Wajasiliamali na kwa kumuunga mkono Rais Magufuli. Mwenyezi Mungu azidi kumbariki Msanii Harmonize." Alisema DC Waryuba.

Mnamo Machi 16, 2019 msanii Harmonize alitoa ahadi ya kuwanunulia vitambulisho kwa Wajasiliamali 50 kwenye mkutano uliofanyika stendi ya mabasi Tandahimba ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Byakanwa alikuwa mgeni rasmi.
IMG_20190325_094511_4.jpeg
IMG_20190325_093805_4.jpeg
IMG_20190325_094234_0.jpeg
IMG_20190325_093657_3.jpeg
IMG_20190325_094301_9.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom