DC wako anatekeleza majukumu yake ipasavyo?

DC wako anatekeleza majukumu yake ipasavyo?

Rtbkazoba

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2016
Posts
261
Reaction score
210
Baada ya kuona mambo kadhaa yanayotia mashaka nimejiuliza swali: Hivi Ma-DC wanatekeleza majukumu yao ipasavyo? Tusaidiane kuwapima kwa kutumia Hati ya Majukumu inayowahusu. Hii hapa.....

===========MAJUKUMU YA MKUU WA WILAYA=================


(i) Kumweka mtu kizuizini kwa muda wa saa 48 mfululizo iwapo atashukiwa kuwa ni mhalifu au anayehatarisha hali ya utulivu na Amani (Sheria ya tawala za mikoa Na 19/1997)

(ii) Kufungisha ndoa za serikali (Law of Marriage Act No 5/1971)

(iii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati yaMkoa inayochambua maombi ya watu wanaotaka kuuza madawa ya sumu (Pharmaceuticals and Poisons Act No 9/1978)

(iv) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuongoza Kamati ya kusikiliza rufani za leseni za biashara mkoani (Business Licensing Authority Act No 25/1972, ib. 1)

(v) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya leseni za vileo (Intoxicating Liquours Act No 28/1968)

(vi) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuteua wakaguzi wa magereza (Prisons Act No 34/1967, ib. 100)

(vii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwashughulikia watu wanaodhaniwa kuwa ni wachawi (Witchcraft Ordinance Cap 18)

(viii) Kuwa mhimili msaidizi wa Halmashauri za Wilaya (Sheria Na 7/1982).

(ix) Kuwa mwenyekiti wa Kamati mbalimbali zitakazoundwa Wilayani.

(x) Kuhudhuria vikao vya Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kamamjumbe

(xi) Kushughulikia malalamiko ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi

(xii) Kumsaidia Mkuu wa Mkoa katika kuzisimamia Halmashauri za Wilaya na kuhakikisha kuwa zinatoa huduma nzuri kwa wananchi na kwa ufanisi

(xiii) Kuziwekea Halmashauri za Wilaya mazingira mazuri na kuhakikisha kuwa zinatekeleza majukumu yake kulingana na sera za serikali.

(xiv) Kutekeleza majukumu yote atakayopewa kisheria au kukasimiwa na Mkuu waMkoa.
 
akitimiza hayo majukumu hawezi kuonekqna kwa wananchi maana mengi ni ya kiofisi
 
Huku Iramba ni kama hayupo kabisa. Toka ateuliwe juzi ndio nimemuona akipogoma tu baada ya wachimbaji wa dhahabu kuchimba chini ya nguzo za umeme mkubwa. Sijawahi hata kusikia anahamasiha shughuli za maendeleo au basi hata kutunza mazingira kwa kupanda miti. He one of those who sit and revolve in office chairs
 
Wakuu wa wilaya na Mkoa wanachotimiza kwa 100% ni kipengele cha kwanza tu.Mengine yote ni zero na chenyewe ni kwa sababu ya VISASI,CHUKI,UBAGUZI na WIVU
 
Mbona ni kama anamfanyia kazi mkuu wa mkoa? sasa mkuu wa mkoa kazi zake ni zipi?
 
aisee.. hiki cheo hakistahili kuwepo, ni bora kikafutwa, hakina tija na sioni umuhimu wake, wamekalia kuvuruga wananchi!
uvccm ndio wanajificha huko mkuu. Ukianzisha mada ya kuwa dc na rc wasiwepo upinzania ni mkubwa balaa. Kufanikisha ni mpaka tupate rais wa nchi sio hawa wa chama cha ccm
 
Utajuwaje kama anafanya kazi ipasavyo wakati hakuna semina elekezi?
 
Sasa hiyo namba VII yeye kama DC anatekeleza vipi so wanasema serikali haiamini uchawi!!!!
 
Back
Top Bottom