DC Magu aagiza walimu kufanya usafi shule zao kila Jumamosi

Richruge

Member
Jun 7, 2011
67
12
DC Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza amewaagiza walimu wote kufanya usafi katika vituo vyao vya kazi kuanzia saa kumi na mbili na nusu asubuhi mpaka saa nne asubuhi kila Jumamosi ya kila wiki kuanzia kesho na mahudhurio yatakuwa yanachukuliwa.

My take: Mwl anaye amka kila siku asubuhi Jumatatu mpaka Ijumaa, bado ana kazi ngumu ya kuhangaika na watoto kwa siku hizo za kazi, Unamwambia arudi tena jumamosi saa kumi na mbili na nusu afanye usafi, atapata wapi muda wa kupumzika?

Tuwahurumie hawa watu nao ni binadamu wanahitaji muda wa kuandaa na kupumzisha vichwa!
 
Mbali na hayo pia mwalimu inabidi aandae mitihani ya test. Mm nadhani angewapa kazi kutokana na taaluma zao. Kwa mfano angeweka angalizo la shule itakayoongoza kwa kufeli ata dili nayo. Hayo ya usafi mimi sijui
 
Thats not fair, lakini pia ni upuuzi kabisa kwa mtu mwenye wadhifa huo kwa jamii yake kutoa order ya kijinga kama hyo. achunguzwe vzur vyeti vyake vya elimu.
 
Hatufai kuwa kiongozi. Ningependa taratibu za kumfukuza kazi zingefuatwa ili ndugu zetu wengine wenye sifa stahiki waajiliwe.

Kama kiongozi wa kuigwa .hatuwezi IGA ujinga huo. Mpuuzi sana...
 
Kila DC anataka alinde nafasi yake ili aendelee kwepo kwenye serikali ya JPM lakini kwa hali hii sio haki.
 
Nona kila DC anajaribu kujihakikishia nafasi kupitia Walimu. Nafikiri ni wakati muafaka kwa chama cha walimu kutoa tamko ili haya mambo yaishe, na kama kuna jambo utaratibu ufuatwe.
 
Nchi hii ina mijitu ya hovyo kabisa huyo dc sina uhakika kama ni mzima kichwani,kwani mkataba wa kazi unasemaje?yaani hayo yote ili magu asimtengue,raisi wangu kama ningepata muda wa kukushauri ni wazi ma dc wa namna hii wangeshahama nchi,wenzake wanaangaika namna ya kusaidia walimu wengine wanakuja na mawazo ya kitoto.
 
kama hii habari ni ya kweli huyo dc ni mtu wa hovyo na sidhani kama mh magu ataendelea nae,hii ni aibu kubwa sana.
 
Kwa hayo aliyosema,dhahiri huyo DC ni zero kichwani.Akapimwe maana anachofanya hakijui na kukitambua.
 
Nona kila DC anajaribu kujihakikishia nafasi kupitia Walimu. Nafikiri ni wakati muafaka kwa chama cha walimu kutoa tamko ili haya mambo yaishe, na kama kuna jambo utaratibu ufuatwe.
Hivi chama cha walimu kipo kweli? Siamini...
Mwalimu afanye usafi.... na mwanafunzi afanye nini???
 
CWT Ikakaaa kimya bila kukemea hili kwa nguvu zote nitashangaa.

Mke wangu ni Mwl kaambiwa arudi kazini jmos kujitolea kufundisha! Amekataa kwani jmos sio siku ya kazi na sheria ya ajira imeweka utaratibu wa kufanya Kazi mda wa ziada. Sasa kuzua bifu na mkuu wa shule
 
Kiongozi hilo dude cwt linapatikana wapi?lilishawahi kumsaidia nani?


Hilo lli CWT ni lichama la kutafutia nyadhifa tuu maana utasikia katibu mkuu wa CWT Taifa kateuliwa kuwa MKUU wa wilaya lenyewe li CWT linaombea walimu wapate KESI ndo liseme lina kusaidia


Hapa napo kuna majipu ya mgongoni hayatoki mpaka apatikane wa kuyashughurikia

Wameanzisha Bank ya WALIMU lakini mpaka leo watu hawajapewa vyeti vyao vyaununuzi wa HISA



PUUUUUUU bora LIFE
 
Back
Top Bottom