DAWASCO hizi mita zenu mpya mmezileta kutukomoa

lauzi96

JF-Expert Member
Jul 10, 2014
422
797
Hizi meter kabla bi mkubwa hajafungiwa nilikuwa nnalipa ikizidi sana elf 18 hila mwezi uliyopita wameweka mita mpya ya maji ni hatari ile nnadhani haitumii maji kuzunguka labda itakuwa ya solar maana mzee kanipigia simu bili imetoka mwezi mmoja elf 35 halafu nyumba wanakaa watu 2 tu nimetoka mishe nikapitia kuwacheck nikaonyeshwa hyo mita nikafunga mabomba yote nnaona mita bado inazunguka pale pale kwenye mita kuna koki yake ile nyeusi ya plastic nikafunga lakini mishale ya mita inazunguka kama kuna wahusika hebu tuambiane hizo meter zinatumia maji au za solar.
 
Hawa jamaa ni wa ajabu sana mkuu. Hizi mita nafikiri zinatuhujumu watumiaji.
Nimeletewa bill ya ajabu sana mwezi huu.
 
Bora wewe.sie tunaletewa si chini ya laki.
 
Mimi nasoma hadi units kutoka mwezi hadi mwezi.cha ajabu bili naletewa kubwa.
 
makumbuka kaka yangu siku moja alinilaumu sana, kwamba tumetumia Maji kiasi kwamba billi ikaja kuwa kubwa. maana matumizi yetu hayakufanana kabisa na bili ya maji. kumbe kuna jambo kah!
 
Hawa jamaa wezi sana, majuzi wameniletea bill ya ajabu nikawaambia silipi, haiwezekani waniletee bill kubwa kuzidi matumizi yangu, bill ya nyumba wanayoishi watu watano inakuwa kama bill ya taasisi?
 
Hawa jamaa ni wa ajabu sana mkuu. Hizi mita nafikiri zinatuhujumu watumiaji.
Nimeletewa bill ya ajabu sana mwezi huu.
Mimi nawalaumu sana hawa jamaa wa mizani na vipimo, wanakimbizana na Rumbesa wanatuacha huku tunaibiwa bila kupenda! Hizi mita huwa wamezilegeza hawa jamaa wa mamlaka za maji na hili ni janga kwa nchi nzima. Mkuu kama mko Dar hebu fuatilieni utaratibu wa kuzifania calibration hizo mita. Niliwapigia simu jamaa wa mizani na vipimo wakasema hiyo huduma iko makao makuu ya ofisi zao hapo Dar, eti mteja akihitaji huduma hiyo inabidi afunue mita yake na kuipeleka Dar. Huu ni wizi, eti kwangu natumia mapipa 175 kwa mwezi, haiwezekani nitumie mapipa 6 kwa siku huu ni wizi!
 
Hawa jamaa wezi sana, majuzi wameniletea bill ya ajabu nikawaambia silipi, haiwezekani waniletee bill kubwa kuzidi matumizi yangu, bill ya nyumba wanayoishi watu watano inakuwa kama bill ya taasisi?
Aisee haya mambo kuna namna inabidi wahusika wayatolee ufafanuzi otherwise tupate kitu mbadala sio kwa kutukamua huko na units ambazo hatuzitumii
 
Huku knyama tuna koma tangu mwezi dec wiki kabla ya xmas hatuna maji kisingizio wanafunga mabomba mapya mpaka leo hatuja wahi kuona maji,ngoja tusubiri bill ya dec itasoma vp safari hii
 
Ni kweli kabisa, nilishuhudia , mabomba yote yamefungwa lakini mita inazunguka, kila mtu anazilalamikia hizo mita, yaani haya mashirika ya umma yamekaa kibiashara na kumyonya mwananchi, si kumpa unafuu.
 
Poleni sana tena ni vizuri kabisa. Napenda izidi zaidi na zaidi tena iwe maradufu kabisa.
 
Kwangu nilikuwa natumia maji yasizidi shs 30,000 sasa hivi mara mbili yake. Nimelalamika wakabadilisha karibu eneo lote lakini bado wananchi wanakamliwa kama kawaida. Seriously hizi mita ni balaaaaaaa.
 
Duwasa:Dom hiyo.Nimejaribu kumlipia mama yangu bili ya maji kwa Tigo pesa lakini nimeshindwa.Hampo kwenye majina ya kampuni yaliyoorodheshwa!Ningependa niwe natumia njia hii kulipa bili kuliko kumsumbua bi mkubwa kwenda kulipa.Labda ni mimi ndio nakosea?Malipo kwa njia ya simu yanaokoa muda na ni salama pia.
 
Mimi nawalaumu sana hawa jamaa wa mizani na vipimo, wanakimbizana na Rumbesa wanatuacha huku tunaibiwa bila kupenda! Hizi mita huwa wamezilegeza hawa jamaa wa mamlaka za maji na hili ni janga kwa nchi nzima. Mkuu kama mko Dar hebu fuatilieni utaratibu wa kuzifania calibration hizo mita. Niliwapigia simu jamaa wa mizani na vipimo wakasema hiyo huduma iko makao makuu ya ofisi zao hapo Dar, eti mteja akihitaji huduma hiyo inabidi afunue mita yake na kuipeleka Dar. Huu ni wizi, eti kwangu natumia mapipa 175 kwa mwezi, haiwezekani nitumie mapipa 6 kwa siku huu ni wizi!
Ni kweli kabisa mkuu. Nitafuatilia hili suala la mizani na Vipimo wiki hii,halafu nitaleta mrejesho hapa.
Hii ni hujuma ya wazi.
 
Back
Top Bottom