Shida ni kuondoa myomas kwani naona ndiyo yanayobleed. Naelewa sana menopause na stage zoote nilishapitia.
Asante kwa ushauri. Hizo dalili nilizowekea red ndizo nilizonazo. Ultra sound nimeshafanya na nikaambiwa myomas zipo kwenye mdomo wa kizazi. Nikaelezwa kuna option mbili: kufanyiwa upasuaji na kutoa uterus yote kwani mie sihitaji mtoto tena na hata umri hauniruhusu au kusubiri nifike menopause kisha myomas zitacolapse kwani hormons za estrogen za kuzilisha zitaguwa hazizalishwi tena. Niliamua kutumia option ya pili ya kungoja menopause kwani wakati huo nilikuwa na miaka 48 na dalili zote za menopause nilikuwa nazipata. Huu ni mwaka wa 4 na mambo ya hot flushes na adha nyingine za menopause zimeshapita. Ajabu bado nableed, tena sana. Ndo maana nauliza je niende hospitali gani au nimwone daktari yupi anipatie hivyo vidonge ulivyosema naweza kutumia ili uvimbe uishilie mbali? Naogopa na sitaki kupasuliwa.i really doubt definition yako ya menopause(ambayo hujaisema ingawaje niliulizia hapo mwanzo)..Hata hivyo ningependa kusema,
Myoma
Ni aina ya uvimbe utokeao katika misuli, na ile itokeayo katika kizazi huitwa Uterine myoma...
Takwimu nyingi huonyesha kuwa tatizo hili la uvimbe hutokea kwa wanawake wenye umri wa kuweza kushika mimba(reproductive age),hata hivyo asilimia chache/ndogo sana hutokea kwa wale waliomaliza.
Dalili:
-Kukojoa(kwenda haja ndogo) mara kwa mara.
-Damu kutoka nyingi wakati wa hedhi au kati ya mzunguko na mzunguko.
-Maumivu makali sana wakati wa hedhi, maeneo ya tumbo na kiunoni (ingawaje maumivu wakati/kabla ya hedhi ni kawaida).
-Dalili za upungufu wa damu(kizunguzungu, kuchoka haraka, kuhisi mapigo ya moyo kwenda kasi isivyo kawaida).
-Mimba kutoka(kuharibika).
-Ugumba/utasa.
Vipimo mbali mbali vinaweza kufanyika na Picha ya tumbo (Abdominal Ultrasound) na USS za aina nyingine huweza kugundua aina ya uvimbe/vivimbe, ukubwa, sehemu gani vilipo katika tumbo la uzazi n.k
Tiba:
Njia za kupunguza/kuondoa vivimbe hutegemeana na aina ya uvimbe,tabia yake, umri wa mgonjwa, utashi wa kuweza kuwa na watoto, kama ana ugonjwa/tatizo jingine tofauti na hilo(mf.matatizo ya mfumo wa damu, moyo n.k)
Hivyo mgonjwa anaweza kupatiwa dawa(vidonge) bila upasuaji, dawa na kisha upasuaji au upasuaji moja kwa moja.
Ushauri:
Ni vyema kufanya uchunguzi hospitalini, na kupata elimu kutoka kwa daktari wako katika kuamua njia gani inayofaa KWAKO.
nishauri nikamwone Dr yupi?mamayeyo,
Kwa daktari mzuri na makini, atakuruhusu kuendelea na option ya kuondoa tumbo la kizazi..kwa umri wako, hitaji la kutopata mtoto..Dawa zina madhara pia, sasa ni kwanini uendelee kupata madhara tokezi(side effects) wakati unaweza kupata tiba nzuri...Pia option ya "wait and see" menopause inaweza chukua miaka miwili hadi mitano toka umri wako wa sasa, so tatizo laweza kuendelea bado!
Anyway, bado sababu ya Patient's wish still holds water..so ningekushauri nenda hospitali(private ofcourse), opt
nishauri nikamwone Dr yupi?
Dada asante kwa ushauri Kweli mateso ninayoyapata napaswa kabisa kufanyiwa upasuaji. Roho yangu bado inakusanya courage kwani nina kawoga fulani hivi. Miaka ya nyuma kidogo rafiki yangu alifanyiwa upasuaji huo, baada ya siku moja pressure ikapanda akafariki. Sijui kama hicho ndo kinaniogopesha au nini, lakini nina kawoga fulani tu.dada,kwa nini usifanye operesheni tu.mbona siku hizi sio ya kutisha sana.mambo ya ku bleed hayo sio mazuri
Pole sana Mama Yeyo. Sijui ni kwa nini hutaki kupasuliwa kwani huna sababu za kuogopa kupasuliwa na kuondolewa kizazi, kwani kama ulivyosema hutaraji kupata watoto tena. Kuna jambo moja naogopa lisije kukutokea;nalo ni uwezekano wa vivimbe hivyo kubadilika na kuwa malignant yaani kugeuka kuwa kansa ya kizazi ambayo madhara yake ni makubwa mno! Nakushauri ukubali, ufanyiwe operesheni yaishe kwani wahenga walishasema heri nusu shari kuliko shari kamili.Asante kwa ushauri. Hizo dalili nilizowekea red ndizo nilizonazo. Ultra sound nimeshafanya na nikaambiwa myomas zipo kwenye mdomo wa kizazi. Nikaelezwa kuna option mbili: kufanyiwa upasuaji na kutoa uterus yote kwani mie sihitaji mtoto tena na hata umri hauniruhusu au kusubiri nifike menopause kisha myomas zitacolapse kwani hormons za estrogen za kuzilisha zitaguwa hazizalishwi tena. Niliamua kutumia option ya pili ya kungoja menopause kwani wakati huo nilikuwa na miaka 48 na dalili zote za menopause nilikuwa nazipata. Huu ni mwaka wa 4 na mambo ya hot flushes na adha nyingine za menopause zimeshapita. Ajabu bado nableed, tena sana. Ndo maana nauliza je niende hospitali gani au nimwone daktari yupi anipatie hivyo vidonge ulivyosema naweza kutumia ili uvimbe uishilie mbali? Naogopa na sitaki kupasuliwa.