mamayeyo
Senior Member
- Apr 4, 2012
- 167
- 132
Wadau, sina hakika kama swali hili limeshaulizwa humu au vipi. Naomba msaada wenu. Nina miaka zaidi ya 50 na nina myomas kwenye kizazi yananisumbua sana na yanasababisha nisifike menopause. Nimeshauriwa nifanyiwe upasuaji yaondolewe lakini roho yangu haitaki kabisa operation. Je nani anafahamu mahali nitapata dawa za kufanya yasinyae yenyewe na kwisha kabisa bila operation? . Nimekunywa dawa za Kimasai, Kichina na Kihindi lakini hali inazidi kuwa mbaya. Tafadhali naomba msaada kwa yeyote anayejua pa kupata dawa anielekeze.