Dawa ya kuondoa myomas kwenye kizazi bila ya operation inapatikana wapi?

mamayeyo

Senior Member
Apr 4, 2012
167
195
Wadau, sina hakika kama swali hili limeshaulizwa humu au vipi. Naomba msaada wenu. Nina miaka zaidi ya 50 na nina myomas kwenye kizazi yananisumbua sana na yanasababisha nisifike menopause. Nimeshauriwa nifanyiwe upasuaji yaondolewe lakini roho yangu haitaki kabisa operation. Je nani anafahamu mahali nitapata dawa za kufanya yasinyae yenyewe na kwisha kabisa bila operation? . Nimekunywa dawa za Kimasai, Kichina na Kihindi lakini hali inazidi kuwa mbaya. Tafadhali naomba msaada kwa yeyote anayejua pa kupata dawa anielekeze.
 
hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,600
1,225
Mkuu mamayeyo,
Inawezekana uvimbe ulionao/uliyonayo ni mkubwwa/mikubwa kiasi cha kuhitaji upasuaji(operation)...sijaelewa vizuri, kwani wewe menopause unaelewa ni nini/unaielewaje? Na je, shida ni kutaka kufika menopause kwa kuondoa uvimbe(myomas)?
 
Last edited by a moderator:

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,600
1,225
Mkuu mamayeyo,
Inawezekana uvimbe ulionao/uliyonayo ni mkubwwa/mikubwa kiasi cha kuhitaji upasuaji(operation) ndiyo maana ukashauriwa hivyo...kabla ya yote, sijaelewa vizuri, kwani wewe menopause unaelewa ni nini/unaielewaje? Na je, shida ni kutaka kufika menopause kwa kuondoa uvimbe(myomas)?
 
Last edited by a moderator:

mamayeyo

Senior Member
Apr 4, 2012
167
195
Shida ni kuondoa myomas kwani naona ndiyo yanayobleed. Naelewa sana menopause na stage zoote nilishapitia.
 
hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,600
1,225
Shida ni kuondoa myomas kwani naona ndiyo yanayobleed. Naelewa sana menopause na stage zoote nilishapitia.
i really doubt definition yako ya menopause(ambayo hujaisema ingawaje niliulizia hapo mwanzo)..Hata hivyo ningependa kusema,

Myoma
Ni aina ya uvimbe utokeao katika misuli, na ile itokeayo katika kizazi huitwa Uterine myoma...

Takwimu nyingi huonyesha kuwa tatizo hili la uvimbe hutokea kwa wanawake wenye umri wa kuweza kushika mimba(reproductive age),hata hivyo asilimia chache/ndogo sana hutokea kwa wale waliomaliza.

Dalili:
-Kukojoa(kwenda haja ndogo) mara kwa mara.
-Damu kutoka nyingi wakati wa hedhi au kati ya mzunguko na mzunguko.
-Maumivu makali sana wakati wa hedhi, maeneo ya tumbo na kiunoni (ingawaje maumivu wakati/kabla ya hedhi ni kawaida).
-Dalili za upungufu wa damu(kizunguzungu, kuchoka haraka, kuhisi mapigo ya moyo kwenda kasi isivyo kawaida).
-Mimba kutoka(kuharibika).
-Ugumba/utasa.

Vipimo mbali mbali vinaweza kufanyika na Picha ya tumbo (Abdominal Ultrasound) na USS za aina nyingine huweza kugundua aina ya uvimbe/vivimbe, ukubwa, sehemu gani vilipo katika tumbo la uzazi n.k

Tiba:
Njia za kupunguza/kuondoa vivimbe hutegemeana na aina ya uvimbe,tabia yake, umri wa mgonjwa, utashi wa kuweza kuwa na watoto, kama ana ugonjwa/tatizo jingine tofauti na hilo(mf.matatizo ya mfumo wa damu, moyo n.k)
Hivyo mgonjwa anaweza kupatiwa dawa(vidonge) bila upasuaji, dawa na kisha upasuaji au upasuaji moja kwa moja.

Ushauri:
Ni vyema kufanya uchunguzi hospitalini, na kupata elimu kutoka kwa daktari wako katika kuamua njia gani inayofaa KWAKO.
 
Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,697
1,250
Anyway,inawezekana kweli kuna uwezekano wa kutumia mitishamba ukapona,ila mimi huko siwezi kusema chochote maana sio taaluma yangu. Lakini mi kwa haraka haraka ninaweza kusema sasa umefika wakati wa kuprove failure ya hizo dawa ulizosema,maana kama umetumia dawa aina zote hizo na bado hali inazidi kuwa mbaya,kwa nini nisiseme unapoteza muda wako unapoendelea kutumia dawa hizo?

Inavyoelekea wewe una uelewa mzuri juu ya jambo hili(kama ulivyosema),ni kwa nini sasa unakosa uelewa wa kujua madhara ya kuendelea kulea tatizo hili?Hebu tuwe serious sasa. Kwa umri wako na ukubwa wa tatizo lako,sijaona sababu ya msingi ya kwa nini unakataa ushauri wa watalamu(Gynaecologists).Laiti kama ungejua madhara ya kuendelea kukaa na tatizo hili,naamini ungishachuka hatua zinazostahili muda mrefu sana. Lakini kwa kuwa umeamua kuacha njia sahihi na ya kuaminika,wewe umefuata njia unazoona mwenyewe zinafaa,fine. Mi nakutakia kila la kheri huko uendako mama.
 
mamayeyo

Senior Member
Apr 4, 2012
167
195
i really doubt definition yako ya menopause(ambayo hujaisema ingawaje niliulizia hapo mwanzo)..Hata hivyo ningependa kusema,

Myoma
Ni aina ya uvimbe utokeao katika misuli, na ile itokeayo katika kizazi huitwa Uterine myoma...

Takwimu nyingi huonyesha kuwa tatizo hili la uvimbe hutokea kwa wanawake wenye umri wa kuweza kushika mimba(reproductive age),hata hivyo asilimia chache/ndogo sana hutokea kwa wale waliomaliza.

Dalili:
-Kukojoa(kwenda haja ndogo) mara kwa mara.
-Damu kutoka nyingi wakati wa hedhi au kati ya mzunguko na mzunguko.
-Maumivu makali sana wakati wa hedhi, maeneo ya tumbo na kiunoni (ingawaje maumivu wakati/kabla ya hedhi ni kawaida).
-Dalili za upungufu wa damu(kizunguzungu, kuchoka haraka, kuhisi mapigo ya moyo kwenda kasi isivyo kawaida).
-Mimba kutoka(kuharibika).
-Ugumba/utasa.

Vipimo mbali mbali vinaweza kufanyika na Picha ya tumbo (Abdominal Ultrasound) na USS za aina nyingine huweza kugundua aina ya uvimbe/vivimbe, ukubwa, sehemu gani vilipo katika tumbo la uzazi n.k

Tiba:
Njia za kupunguza/kuondoa vivimbe hutegemeana na aina ya uvimbe,tabia yake, umri wa mgonjwa, utashi wa kuweza kuwa na watoto, kama ana ugonjwa/tatizo jingine tofauti na hilo(mf.matatizo ya mfumo wa damu, moyo n.k)
Hivyo mgonjwa anaweza kupatiwa dawa(vidonge) bila upasuaji, dawa na kisha upasuaji au upasuaji moja kwa moja.

Ushauri:
Ni vyema kufanya uchunguzi hospitalini, na kupata elimu kutoka kwa daktari wako katika kuamua njia gani inayofaa KWAKO.
Asante kwa ushauri. Hizo dalili nilizowekea red ndizo nilizonazo. Ultra sound nimeshafanya na nikaambiwa myomas zipo kwenye mdomo wa kizazi. Nikaelezwa kuna option mbili: kufanyiwa upasuaji na kutoa uterus yote kwani mie sihitaji mtoto tena na hata umri hauniruhusu au kusubiri nifike menopause kisha myomas zitacolapse kwani hormons za estrogen za kuzilisha zitaguwa hazizalishwi tena. Niliamua kutumia option ya pili ya kungoja menopause kwani wakati huo nilikuwa na miaka 48 na dalili zote za menopause nilikuwa nazipata. Huu ni mwaka wa 4 na mambo ya hot flushes na adha nyingine za menopause zimeshapita. Ajabu bado nableed, tena sana. Ndo maana nauliza je niende hospitali gani au nimwone daktari yupi anipatie hivyo vidonge ulivyosema naweza kutumia ili uvimbe uishilie mbali? Naogopa na sitaki kupasuliwa.
 
hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,600
1,225
mamayeyo,

Kwa daktari mzuri na makini, atakuruhusu kuendelea na option ya kuondoa tumbo la kizazi..kwa umri wako, hitaji la kutopata mtoto..Dawa zina madhara pia, sasa ni kwanini uendelee kupata madhara tokezi(side effects) wakati unaweza kupata tiba nzuri...Pia option ya "wait and see" menopause inaweza chukua miaka miwili hadi mitano toka umri wako wa sasa, so tatizo laweza kuendelea bado!

Anyway, bado sababu ya Patient's wish still holds water..so ningekushauri nenda hospitali(private ofcourse), opt
 
Last edited by a moderator:

mamayeyo

Senior Member
Apr 4, 2012
167
195
mamayeyo,

Kwa daktari mzuri na makini, atakuruhusu kuendelea na option ya kuondoa tumbo la kizazi..kwa umri wako, hitaji la kutopata mtoto..Dawa zina madhara pia, sasa ni kwanini uendelee kupata madhara tokezi(side effects) wakati unaweza kupata tiba nzuri...Pia option ya "wait and see" menopause inaweza chukua miaka miwili hadi mitano toka umri wako wa sasa, so tatizo laweza kuendelea bado!

Anyway, bado sababu ya Patient's wish still holds water..so ningekushauri nenda hospitali(private ofcourse), opt
nishauri nikamwone Dr yupi?
 
kisukari

JF-Expert Member
Jul 16, 2010
4,545
2,000
dada,kwa nini usifanye operesheni tu.mbona siku hizi sio ya kutisha sana.mambo ya ku bleed hayo sio mazuri
 
Chiya Chibi

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
484
195
Dawa zote umeshamaliza, Kafanye operation kama ulivyoelekezwa, usijisumbue kutafuta dawa. Operation ndo dawa pekee uliyobakiza.
 
mamayeyo

Senior Member
Apr 4, 2012
167
195
dada,kwa nini usifanye operesheni tu.mbona siku hizi sio ya kutisha sana.mambo ya ku bleed hayo sio mazuri
Dada asante kwa ushauri Kweli mateso ninayoyapata napaswa kabisa kufanyiwa upasuaji. Roho yangu bado inakusanya courage kwani nina kawoga fulani hivi. Miaka ya nyuma kidogo rafiki yangu alifanyiwa upasuaji huo, baada ya siku moja pressure ikapanda akafariki. Sijui kama hicho ndo kinaniogopesha au nini, lakini nina kawoga fulani tu.
 
REX

JF-Expert Member
Mar 24, 2012
331
195
Myomas au uterine fibroids are slow growing benign tumours that develops from smooth muscle cells in the myometrium
They are the most common benign tumours and most of the time remain small and asymptomatic and prevalence increases in women aging 30-50yrs.
Risk factors for development of uterine leiomyoma includes
1.black race.being black you have a 50% risk of developing myoma
2.hormonal fluctuations particularly estrogen
3.dietary deficiency of poly unsaturated fatty acids, importand anthoxidants like vitamin c,vit E and vit A and lack of important co-factors in the body like zinc,selenium.
3.Excessive and irrational use of alcohols,red meet and unhealthy life styles
4.poor or bad eating habits.
The main stay of treatment in advanced myomas is surgery otherwise we treat conservatively following the protocol below in order of preference
1.watchful waiting
2.phytotherapy
3.medical treatment
4.surgical treatment.
To date the cause of uterine myoma is not known but its thought to be related to the above mentioned risk factors and even with surgery that is thought to be the gold standard the rate of recurency is high and surgeqy caries its own risks.
Currently people can manage and even cure completely uterine leiomyoma without surgery using special diets that are natural and body friendly
Am willing to assist those who are ready and they will strictly follow my plan.
My plan is worthy 350,000 to start and tumor is gone away.we have various testimonies from those who initialy had leiomyoma and now are tumors free.
Dont hesitate cal me at 0752720276.
 
luhala

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
412
0
Asante kwa ushauri. Hizo dalili nilizowekea red ndizo nilizonazo. Ultra sound nimeshafanya na nikaambiwa myomas zipo kwenye mdomo wa kizazi. Nikaelezwa kuna option mbili: kufanyiwa upasuaji na kutoa uterus yote kwani mie sihitaji mtoto tena na hata umri hauniruhusu au kusubiri nifike menopause kisha myomas zitacolapse kwani hormons za estrogen za kuzilisha zitaguwa hazizalishwi tena. Niliamua kutumia option ya pili ya kungoja menopause kwani wakati huo nilikuwa na miaka 48 na dalili zote za menopause nilikuwa nazipata. Huu ni mwaka wa 4 na mambo ya hot flushes na adha nyingine za menopause zimeshapita. Ajabu bado nableed, tena sana. Ndo maana nauliza je niende hospitali gani au nimwone daktari yupi anipatie hivyo vidonge ulivyosema naweza kutumia ili uvimbe uishilie mbali? Naogopa na sitaki kupasuliwa.
Pole sana Mama Yeyo. Sijui ni kwa nini hutaki kupasuliwa kwani huna sababu za kuogopa kupasuliwa na kuondolewa kizazi, kwani kama ulivyosema hutaraji kupata watoto tena. Kuna jambo moja naogopa lisije kukutokea;nalo ni uwezekano wa vivimbe hivyo kubadilika na kuwa malignant yaani kugeuka kuwa kansa ya kizazi ambayo madhara yake ni makubwa mno! Nakushauri ukubali, ufanyiwe operesheni yaishe kwani wahenga walishasema heri nusu shari kuliko shari kamili.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom