Samahan,ndugu zangu !kuna unene wa asili? Kwamba hata utumia njia zote haiwezekani pungua*
Mimi nilikua nawo huo wa asili, ila nimepmbana mpaka nimepungua sana, hamna dawa ya kupunguza unene tuache kudanganyana, mbinu ni moja tu, mazoezi na kupunguza wanga basi.
Mazoezi haswa ya kukimbia, sema watu wengi hukata tamaa mapema, hutegemea kupunguza unene ndani ya wiki moja, hii ni shughuli ambayo unapaswa kuwa mvumilivu, pambana, kimbia mara nne kwa wiki, ila anza kwa kutembea tembea kisha ongeza kukimbia taratibu mdogo mdogo, usianze kwa mihemko.
Ilinichukua mwaka mmoja kupunguza kilo 35kgs, nilikomaa nikafanya kukimbia kama sehemu ya maisha yangu, siku ikipita sijakimbia yaani mwili huzingua, huwa nahisi hovyoo sana.
Pia punguza msosi wa jioni, kama lazima, basi kula matango, hakikisha kuna masaa kama kumi hivi hujala kitu, yaani chakula cha mwisho kula 6pm kuanzia hapo usile kitu mpaka asubuhi.
Kumbuka kuwa mvumilivu usiyekata tamaa, kuna wakati nilikua nayafanya yote hayo mwezi unaisha nikipima nakuta nimeongeza uzito badala ya kupungua. Lakini sikukata tamaa, maana mwili huwa unajua namna ya kujilinda, kuna wakati unagoma haupungui kitu licha ya yote hayo, wakati huo huwa unafanya balance fulani za kujilinda, unatunza mafuta bila kuyatumia, ila ghafla utashangaa ipo wiki utapungua hata kilo tatu kwa mpigo.
Mwezi wote huu nimepambana sana wiki zimeenda kila nikipima nakuta nimeongeza, ila leo nimepima nikakuta nimepungua kilo moja ghafla, na wala sio kwamba nimebadilisha aina ya mazoei au msosi, yaani mwili wenyewe unakwenda utakavyo.