David Kafulila: Namshauri Rais azifikishe kampuni zote hizo kwenye mahakama ya kimataifa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
.Naipongeza Kamati kwa kazi iliyotukuka iliyojaa majaribu ya rushwa kubwa kwani kampuni nyingi madini, mafuta na gas duniani zina sifa hiyo kama alivyopata kusisitiza Profesa Joseph Stirglitz gwiji la uchumi na utandawazi duniani.

2.Zaidi hatua alochukua Rais kuhusu uharamia huu katika sekta ya madini inapaswa kuungwa mkono na kila mzalendo kwani imekuwa hoja ya upinzani na kila mzalendo kwa miaka mingi iliyoishia kubezwa na kupuuzwa.

3.Rais asiishie kutaka uchunguzi kufanywa dhidi ya watumishi ktk sekta ya madini tu, nchi hii imeoza, uchunguzi ufanywe mpaka ndani ya Idara ya Usalama na vyombo kama TAKUKURU kwani mafisadi hawa waliweka mfumo mzima mfukoni kwa kujenga mahusiano na baadhi ya wanausalama na vyombo vingine vyeti kiuchunguzi.

4.Namshauri Rais aboreshe Idara ya Usalama kwakuwa na kitengo cha ujasusi wakiuchumi(Economic Intelligency) kitakachoweza kumudu kukabiliana na uharamia ktk utoroshaji utajiri wa nchi (illicits flows) kwani nchi inavuja kwa miaka mingi na mtandao wa uharamia huu uliweka sehemu kubwa ya mfumo mfukoni.

5.Kuna haja yakutazama Katiba yetu upya ili ikibainika hata Rais kama alihusika na ufisadi afikishwe kwenye mkondo wa sheria kwani nchi nyingi za Africa zimeoza kwa ufisadi kuanzia Ofisi Kuu, huko ndio vinatoka VIMEMO kuruhusu uharamia wanamna hii.Ni Ushauri wangu kwa Rais aruhusu mchakato wa Katiba ili pamoja na mambo mengine tuangalie mfumo wa Ofisi Kuu kama moja ya chanzo cha uozo na uharamia huu.

6.Nivema Mhe Rais akatambua kwamba kampuni hizi za kimataifa zinaiba duniani kote ikiwemo Ulaya na Marekani, isipokuwa huku kwetu zinaiba zaidi kutokana na sera duni, sheria dhaifu, mifumo ya usimamizi dhaifu na udhaifu wa wanaopewa nafasi kwa ujumla.kukabili tatizo hili lazma kutazama kwa mapana na kutengeneza mfumo madhubuti.

7.Mwisho nimshauri Rais kwamba pamoja na kuchukua hatua hizi za kisheria za ndani, azifikishe kampuni hizi kwenye Mahakama za Kimataifa (Arbitration court) kama inavyotamkwa kwenye mikataba ili kuzidai fidia kwa miaka yote ya Mikataba yao.Mitambo na mali zao zishikiliwe mpaka kesi itapomalizika.Nahili lisisomeke kwamba nikukimbiza wawekezaji bali nikukabili uharamia wa utoroshaji rasilimali ambao hata sheria zakimataifa zinapiga vita.Hili nimuhimu sana.Umma unapaswa kusimama pamoja dhidi ya uharamia huu!
 
hivi hatujajifunza kutoka kamati ya mwakyembe ya richmond?tuweke akiba ya maneno jamani.
 
Ukimchungua Raisi bila shaka utagusa na bataza zima la mawaziri sasa hapo sijui nani atabaki salama maana hata miswaada sidhani kama huwa inaenda Bungeni bila kupitia kwanza kwenye baraza la mawaziri.
 
Back
Top Bottom