Daudi hukujipanga kumuua goliati.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,209
4,406
DAUDI HUKUJIPANGA.

1)kishindo kimesikika,bomu laenda lipuka.
Mboga imeshamwagika,mambo yanaharibika.
Na siri zinafichuka,zile zilizofichika.
Daudi hukujipanga,kumuua Goliati.

2)Mzimu unafufuka,kaburini unatoka.
Yahamka ulozika,yakipaa na kuruka.
Ya wazi yalofichika,goliati ameruka.
Daudi hukujipanga,kumuua goliati.

3)Anga nalo lapasuka,nchi inatetemeka.
Usingizi wahamka,walolala wazinduka.
Nguvu yako yatoweka,ukome kukurupuka.
Daudi hukujipanga,kumuua goliati.

Shairi=DAUDI HUKUJIPANGA
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com
 
kukurupuka ni bomu la maangamizi.ukiondoa pin ya usalama kwenye bomu usiendelee kulichezea !
 
Daudi bashite pole, huruma nakuonea
Koromije polepole, karibu twakungojea
ulijitia kiherehere, jiji ulilivamia
sasa unarudi na ndala, kipi ulicho sahau?

Wewe kweli ni bashite, wala usiweke vyeti
taumbuka kiokote, kichwa zero huna vyeti
ulifoji ukamatwe, haujui hisabati
Umelivamia jiji, karibu mkoromije

Cheo lipewa si haba, sasa mekufika hapa
nakitanzi mejikaba, kwa kuwataja mapapa
misifa uliibeba, sasa mbona unasepa?
Daudi mkoromije, ujitetee mwenyewe

weka magamba mezani, wacha maneno ya kanga
sigeuke hayawani, mahekaluni kutanga
sijifanye punguwani, wewe bado kifaranga
Karibu mkoromije, karibu tulime pamba

ulisomea uvuvi, njoo ziwani tuvue
sangara hata uduvi, biashara tutoboe
Umesha jipaka mavi, husafiki jiondoe
japo zero nayo namba, na chuoni ulidesa

Tamati sisemi sana, kalamu ninaitua
nakuombea kwa rabana, koromije ukitua
nafasi uliyobana, wasomi watachukua
Jipu lako li usoni, magu atalitumbua...
 
Hamna kazi kabisa, mnampenda Mh. Makonda hadi utafikiri inabidi awawekee chakula mezani. Hapa kazi tu, madawa piga chini ma bado

Makonda oyeeeee
 
Daudi bashite pole, huruma nakuonea
Koromije polepole, karibu twakungojea
ulijitia kiherehere, jiji ulilivamia
sasa unarudi na ndala, kipi ulicho sahau?

Wewe kweli ni bashite, wala usiweke vyeti
taumbuka kiokote, kichwa zero huna vyeti
ulifoji ukamatwe, haujui hisabati
Umelivamia jiji, karibu mkoromije

Cheo lipewa si haba, sasa mekufika hapa
nakitanzi mejikaba, kwa kuwataja mapapa
misifa uliibeba, sasa mbona unasepa?
Daudi mkoromije, ujitetee mwenyewe

weka magamba mezani, wacha maneno ya kanga
sigeuke hayawani, mahekaluni kutanga
sijifanye punguwani, wewe bado kifaranga
Karibu mkoromije, karibu tulime pamba

ulisomea uvuvi, njoo ziwani tuvue
sangara hata uduvi, biashara tutoboe
Umesha jipaka mavi, husafiki jiondoe
japo zero nayo namba, na chuoni ulidesa

Tamati sisemi sana, kalamu ninaitua
nakuombea kwa rabana, koromije ukitua
nafasi uliyobana, wasomi watachukua
Jipu lako li usoni, magu atalitumbua...
DAH AISE
 
Daudi bashite pole, huruma nakuonea
Koromije polepole, karibu twakungojea
ulijitia kiherehere, jiji ulilivamia
sasa unarudi na ndala, kipi ulicho sahau?

Wewe kweli ni bashite, wala usiweke vyeti
taumbuka kiokote, kichwa zero huna vyeti
ulifoji ukamatwe, haujui hisabati
Umelivamia jiji, karibu mkoromije

Cheo lipewa si haba, sasa mekufika hapa
nakitanzi mejikaba, kwa kuwataja mapapa
misifa uliibeba, sasa mbona unasepa?
Daudi mkoromije, ujitetee mwenyewe

weka magamba mezani, wacha maneno ya kanga
sigeuke hayawani, mahekaluni kutanga
sijifanye punguwani, wewe bado kifaranga
Karibu mkoromije, karibu tulime pamba

ulisomea uvuvi, njoo ziwani tuvue
sangara hata uduvi, biashara tutoboe
Umesha jipaka mavi, husafiki jiondoe
japo zero nayo namba, na chuoni ulidesa

Tamati sisemi sana, kalamu ninaitua
nakuombea kwa rabana, koromije ukitua
nafasi uliyobana, wasomi watachukua
Jipu lako li usoni, magu atalitumbua...
Ni mshahiri mahiri,
kaka umekamilika.
Sio haja kuhariri,
aya zimekamilika.
Andika uwe tajiri,
Huko mbali utafika.
Kaka umekalika,
Ni mshairi mahiri.
 
Hamna kazi kabisa, mnampenda Mh. Makonda hadi utafikiri inabidi awawekee chakula mezani. Hapa kazi tu, madawa piga chini ma bado

Makonda oyeeeee
Hatumsuti makonda, tumesifiya shairi.
Utenzi tumeupenda, tena tumetafakari.
Piya mzee Ponda, beti ameihiyari.
Tumesifiya shairi, hatumsuti makonda.
 
Hamna kazi kabisa, mnampenda Mh. Makonda hadi utafikiri inabidi awawekee chakula mezani. Hapa kazi tu, madawa piga chini ma bado

Makonda oyeeeee
Hatumsuti makonda, tumesifiya shairi.
Utenzi tumeupenda, tena tumetafakari.
Piya mzee Ponda, beti ameihiyari.
Tumesifiya shairi, hatumsuti makonda.
 
Ni kweli Daudi hakujiandaa kumuua Goliati ila Mungu alikuwa amekusudia Goliati afe kupitia Daudi. Je, nani atashindana na kusudi lake Mungu?
 
Back
Top Bottom