DART yajikita elimu kabla ya mabasi mwendo kasi kuanza

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
DART-18Machi2016.png

Meneja wa Miundombinu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Mhandisi Mohamed Kuganda (kulia), akitoa maelekezo kwa wadau wa usafirishaji jijini Dar es Salaam jana.

Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), imefanya elimu kwa umma juu ya matumizi za miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka kuwa ni kipaumbele kabla ya mabasi kuanza kazi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya wadau wa karibu ya kukagua miundombinu na alama za barabarani ili matumizi yake yawe sahihi, Meneja wa Usimamizi Miundombinu wa Wakala, Mohamed Kuganda, alisema elimu ndiyo italinda miundombinu, usalama wa watumiaji na kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima kwa kila upande.

“Elimu ni muhimu kwa mafanikio ya mradi. Watumiaji wakifanya mambo sahihi, miundombinu itakuwa salama na hawatapata usumbufu wa aina yoyote. Tulichokifanya leo tumechukua watu wa karibu wanaohusika na mambo ya usafirishaji, ili tuelimishane kwa pamoja na elimu hii tutaisambaza kwa umma, hasa watu wanaoendesha vyombo barabarani,” alisema.

Katika ziara hiyo walikuwamo maofisa wa Dart, Polisi Usalama Barabarani, Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) na Mshauri Elekezi (SMEC).

Ukaguzi,ambao unafanywa kwa awamu, ulianzia kituo cha Kimara hadi Morocco.

Mrakibu Mwandamizi wa Polisi ( SSP ), Awadhi Jihad, ambaye ni Kamanda wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni, alisema Jeshi la Polisi litazifanyia kazi changamoto zilizojitokeza.

Kamanda Awadhi alisema alama zipo nyingi katika mradi huo, hivyo watumiaji wanatakiwa kuwa makini ili kuepuka kufanya makosa.

Hata hivyo, aliahidi kwamba polisi wa usalama barabara watajitahidi kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara hasa madereva hata baada ya mradi kaanza kufanya kazi.

Aidha. aliwaonya madereva wa magari, pikipiki, maguta na wanaotumia miundombinu na kuvunja sheria kwa makusudi watachukuliwa hatu kali za kisheria.
Chanzo: Nipashe
 
hiyo ziara italeta ufahamu kwa baadhi ya wadau..
wangetamfuta namna nyngne ya kuelimisha zaidi jamii, mf kwa kuonyesha hz alama ktk vpindi vya tv, wengi wazitambue.
 
Back
Top Bottom