DARING SPIRIT

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
766
Reaction score
1,536
Kwenye maisha kuna kitu kinaitwa “Daring Spirit”(roho ya uthubutu).

Huu ni ule utayari wa kufanya vitu VIGUMU ama VINAVYOHATARISHA bila kuogopa madhara yanayoweza kutokea.

Mara nyingi unapotaka KUVUKA hatua FULANI kwenye maisha yako kwa KASI kubwa lazima uwe nayo hii. Watu wengi kwa sababu ya UOGA wamepoteza FURSA ambazo zingewatoa KIMAISHA.

Hata wewe kuna eneo kwa sasa unahitaji hii kitu. PUNGUZA UOGA na jivike UJASIRI. Fanya hata kama unasikia kuogopa.

HAKUNA KIWANGO KIPYA BILA UJASIRI MPYA. Kuna watu wanasubir ujasiri wako ili wakuunge mkono. Je, wewe unahitaji roho ya uthubutu kwenye kufanya nini?

#Nanauka
 
Nimependa andiko lako na jumbe yako ilivyo nzuri.
Ukitaka kufanikiwa ktk jambo lolote uthubutu (ujasiri) ni jambo la maana sana. Jiepushe na visingizio (vikwazo) haijalishi kikubwa ni kusonga mbele.
Napenda vijana wa umri tofauti kujituma ktk kile wanachokiamini ambacho ni haki na kweli kwa kumaanisha.
Ubarikiwe sana mleta mada nawe nakutakia uishi ktk kusudio linaloendana na mada yako.
 
Amina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…