Darassa, Diamond wanarushiana maneno kimtindo

don88

Member
Jan 22, 2013
53
125
Yasemwayo yapo! Ukiusikiliza kwa makini Wimbo wa Muziki wa mkali wa Hip Hop, Shariff Thabeet ‘Darassa’ kisha ulinganishe matukio na baadhi ya mistari katika nyimbo za Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ utakubaliana nami kuwa, kuna vijembe vimetumika.

Tangu utoke wimbo huo na video ya Muziki ambayo hadi sasa inawatazamaji zaidi ya milioni mbili na nusu kwenye mtandao wa Youtube, wengi wamekuwa wakiusikiliza na kuucheza bila kujua tafsiri ya upande wa pili.

Katika makala haya, nimekuchambulia mistari ya wimbo huo na kulinganisha baadhi ya matukio na nyimbo ambazo Diamond ameziimba.

DARASSA:

Rudi utotoni,

usipotembea utabebwa mgongoni

DIAMOND:

Hapa amegusia bifu la Diamond na Ali Kiba. Inaeleweka kuwa Kiba alikuwa mtu wa kwanza kutoka kimuziki kisha akafuata Diamond. Kiba akiwa staa mkubwa, ndiye aliyemuomba Bob Junior amrekodie Diamond nyimbo zilizomtoa kama Kamwambie katika Studio ya Sharobaro.

Japo chanzo cha bifu lao kuelezwa kuwa ni Diamond kufuta mistari ya Kiba katika wimbo wake wa Lala Salama lakini anapaswa aangalie alipotoka (arudi utotoni).

***

DARASSA:

Wanaota mapembe waongezee mkia

na ukinibeep tu nakupigia

DIAMOND:

Jamaa anamiliki lebo ya muziki ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo mpaka sasa anawamiliki wasanii wanne, Rayvan, Rich Mavoko, Harmonize na Queen Darleen.

Kitendo cha kufanya muziki, kisha kuongeza wasanii mmoja mmoja hadi kufikia wanne imechukuliwa kama kuota mapembe ambapo kwake hajali kwani Diamond akisema anaweza zaidi atamuonesha muziki ulivyo (ukinibeep nakupigia).

****

DARASSA:

And let me make one thing clear

blaa blaa sitaki kusikia

DIAMOND:

Moja ya matukio ambayo yalionekana ni blah blah ni pamoja na lile la Diamond kukutana na Kanye West mwaka jana nchini Marekani.

Alisema kuwa, alikua amekaa kwenye benchi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Los Angeles wa LAX, Kanye West akamfuata na kuomba kupiga picha viatu vyake na hakuwa amegundua mwanzoni kama ni Kanye, alipoangalia juu ndio akamgundua na kupata mshtuko kidogo. Akamuomba kupiga naye picha na kupeana mawasiliano.

***

DARASSA:

Sio simba sio chui sio mamba aaahhhh

ngozi yangu inatosha kujigamba

DIAMOND:

Jina la Simba ni a.k.a anayoitumia kwa muda mrefu akiwa kwenye stage, mitandaoni na hata kwenye nyimbo zake.

Uthibitisho tosha upo katika video yake ya Kidogo aliowashirikisha P-Square mwishoni kabisa, anaonekana akiwa amekaa kwenye kiti huku pembeni yake akiwa na Simba.

Upande wa Darassa ameeleza kuwa, hatumii a.k.a yoyote iwe ya simba wala mamba, jina lake linajiweza.

****

DARASSA:

na sina maneno ya kwenye kanga

ni kazi juu ya kazi yaan bampa tu bampa

DIAMOND:

Ukisikiliza Wimbo wa Nasema Nawe, ni wimbo wa asili ya mduara ambao asilimia kubwa umeimbwa kimafumbo ambayo mara nyingi hutumiwa kwenye kanga, mfano;

‘Ah zingifuri zingifuri, ungezinga mahala ukakaa

Usio mila desturi, usio jua tongozwa ukakataa

Usio hiyana fedhuri, uongo umekujaa

Kujifanya mashuhuri, kumbe chaka umechakaaga

Mwenzako mi ni turufu, si garasa’.

****

DARASSA:

Mzaa unaweza kuzaa kizaazaa

Sinzia na fegi uchome kibanda

Kalale uote ndoto zako za kitanda

si bado tupo macho mida ya wanga

DIAMOND:

Katika Wimbo wa Utanipenda, ameelezea maisha yake halisi ambayo hajayachukulia ‘siriaz’ (mzaa unaoweza kuzaa kizaa zaa) kwa jinsi yatakavyokuja kutokea, mfano ameimba;

Ghafla visenti sina nimerudi Tandale,

Nimeshindwa kulipa bima nimeuza madale,

redio nyimbo wamezima, TV ndo hataree,

Manager umebaki jina hanitaki hata Tale.’

Mingine ni;

Oh bado nimewaza saana, zile tuzo mashauzi airport

Je itapofika tamati mtadiriki hata kuni-post?

Pindi shoo zimekwama, na nikipata sijazi ni mikosi.’

****

DARASSA:

Funga mkanda,

kaza na kamba,

ama ufuate nyayo uchane msamba,

DIAMOND:

Anamlenga hasimu wake ambaye ni Kiba kwamba, afunge mkanda (ajitume), akaze na kamba (asiyumbe) asije kufuata nyayo atajikuta anachanika msamba (kupotea).

***

DARASSA:

Pasua miamba,

pasua anga,

tunasemaga chambua kama karanga

DIAMOND:

Ni jibu la msisitizo linalotoka katika Wimbo wa Salome aliouachia hivi karibuni ambao aliourudia kutoka kwa Saida Karoli na kumjibu kuwa, sasa hivi yeye anapasua tu miamba (shoo za ndani ya nchi) na anga (shoo nje ya nchi) hivyo msemo wa chambua kama karanga uendelee.

Kama utakumbuka katika Salome ya Diamond amesikika akiimba kibwagizo;

“Chambua kama karanga sasa

Chambua kama karanga

Ichambue kama karanga Salome

Chambua kama karanga.”

****

DARASSA:

Maisha na muziki,

acha maneno weka muziki...

DIAMOND:

Kwake maisha ni muziki hapendi mtu anayeongea ongea badala ya kufanya muziki.

****

DARASSA:

Unataka kukimbia na hauna brekii,

what do you expect???

DIAMOND:

Mosi, amefika mbali kimuziki (nje ya Bongo) lakini hiyo haiwafanyi wasanii wengine kushindwa kufika alipo. Mfano tosha alianza kwa kwenda kutoa video nchini Sauz lakini sasa wasanii wengi wanafanya hivyo.

Pili, alikuwa akimaanisha, yeye pamoja na lebo yake wamekuwa wakitoa nyimbo mfululizo kiasi cha kufanya nyimbo zao nyingi kufunikana na kupotea na kushindwa kufikia lengo (kukimbia bila breki).

Mfano, Wimbo wa Matatizo wa Harmonize ulitoka Julai, mwaka jana na mwezi huohuo, Diamond akatoa Wimbo wa Kidogo. Agosti, Rayvan alitoa Natafuta Kiki na mwezi huohuo tena Diamond akatoa Salome. Novemba, mwaka jana, Rayvan alitoa Wimbo wa Sugu lakini mwezi huohuo tena, Rich Mavoko akatoa Wimbo wa Kokoro aliomshirikisha Diamond.

***

DIAMOND:

Watch urself usije ukajiconfuse,

mzuka wa kuruka reggae kwenye blues

DIAMOND:

Amekuwa akisikika kutaka kufanya kolabo nyingi na mastaa wa kimataifa na wengine akisema ameshakamilisha taratibu lakini mwisho wa siku hakuna kitu.

Mfano inadaiwa ameshakamilisha kolabo na staa wa Hip Hop, Rick Ross huku ile ya Rihanna akisema ipo hatua za mwisho. Pia ahadi nyingi za kuibuka na kolabo kubwa za Afrika na wasanii kama Burna Boy, Allaine na Cassper Nyovest huku pia DJ Van wa Morocco pamoja na msanii mkubwa wa Dubai nazo ni maneno tu.

Kwa hiyo ajiangalie asijichanganye maana anaweza kujikuta akiruka Reggae kwenye muziki wa Blues (kuumbuka).

****

DARASSA:

Huna mchuzi,

no excuse,

Maisha yetu ya kila siku kama vile movie

DIAMOND:

Mwaka jana, alimeki ‘headline’ baada ya kutamba kumiliki gari la kifahari lenye thamani ya juu, Rolls Royce. Katika moja ya mahojiano yake alisema;

“Nataka nibadilishe aina ya gari sababu imekua ni muda mrefu, ni muda wa kuwa na gari nililokua nalitamani siku zote, gari la ndoto yangu ni Rolls Royce na litakua na jina la PLATNUMZ na sio namba za kawaida.

“Pia siwezi kuendeshwa nikiwa nimekaa kwenye X6 naonekana kama muhuni tu… ndio maana nataka kutengeneza heshima na Rolls Royce.”

Ukiachana na hilo pia aliwahi kujitamba;

“Nina nyumba South Africa, kwa sababu nina familia huko. Kwa hiyo ni lazima ninunue nyumba South Africa, lakini sina sababu ya kusema ninunue nyumba Marekani. Ninunue nyumba Marekani kwa sababu gani? Kwanza sipapendi, uongozi unajua kabisa.”

Kutokana na mambo mengi yakiwemo hayo, yanaonekana wazi anayapeleka maisha yake kama vile muvi.

****

Vitu vingine havitakag ujuaji,

utajikuta unatandikia watu jamvi,

Kusubiria embe chini ya mnazi,

Kumuelewesha chizi utajipa kazi

DIAMOND:

Utakumbuka Tanzania wapo wasanii wenye uwezo wa kujiongoza lakini wapo chini ya lebo kama Lady Jaydee (Rockstar4000), Ali Kiba (Rockstar4000 na Sony Music) na BarakaThe Prince (Rockstar4000).

Wakati nje ya Afrika, wapo pia mastaa wakubwa wenye uwezo wa kuwa na lebo lakini wanasimamiwa na lebo kama Rihanna (Def Jam na Roc Nation), Big Sean, Rihanna, DJ Khaled, T.I (Roc Nation) ambayo ipo chini ya Jay-Z.

Diamond kila akiulizwa kuhusu kuwa chini ya lebo kubwa jibu lake huwa;

"Wakati nipo Tuzo za BET, Roc Nation walinifuata wakitaka kunisaini nikakataa. Kama ni kupata kolabo na msanii yeyote naweza kupata sababu Kimarekani kolabo siyo stori, hela yako kwani ni biashara, mtu hawezi akakupa bure mfanye nyimbo ili wewe upate hela.”

***

DARASSA:

Wanatamani tupotee kwenye map,

tunapeleka game to the top top,

I that I told you that we don't stop,

we don't stop..."walker"

DIAMOND:

Kitendo cha redio na TV nyingi kupiga nyimbo za lebo yake mara kwa mara na kuacha wasanii wengine ni kama kuwapoteza lakini kwake anasonga na hawezi kusimama.

****

Source: Global Publishers
 

Iringa Native

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
978
1,000
hayo ni madhala ya pombe kijana!muda ulotumia kuoanisha matukio ungekuwa na kazi ungeingiza pesa nzuri

japo mimi nampenda zaidi ALLY KIBA ila natambua kuwa mondi bin laden akifa leo effect yake katika bongo flava itakuwa kubwa sana kama kifo cha late kanumba killivyoathil bongo movie
pia elewa kuwa umemdhalilisha sana dalasa maana ni kama umemaanisha jamaa anamfatilia simba ..

NB:jitahid 2020 uache pombe kama 2015 uliitumia maana inaoneaha maisha ya pombe yamekuvuluga sana!
 

G45

Senior Member
Apr 21, 2016
163
225
Chibu akifa na mziki bongo unakufa nikama kanumba na bongo muvi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom