Dar wafurahia ukombozi maji
WANANCHI zaidi ya 200,000 wa mtaa wa Msakuzi, Kata ya Kwembe Ubungo, wameishukuru serikali na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) kwa kuwafikishia huduma ya majisafi ambayo waliikosa tangu uhuru.
Wakizungumza juzi, wakati wa uzinduzi wa kizimba cha maji katika kata hiyo, Fredy Masha, alisema wanaona ni kama ndoto maji kutoka kwenye bomba, kwa kuwa muda mrefu wamekuwa wakipata shida ya maji na kuingia gharama kubwa kwa kununua maji kwenye Tunaishukuru sana serikali na Dawasa kwa kutuletea maji katika mtaa wetu, tulikuwa tunapata shida sana kila siku tulikuwa fedha nyingi kununulia maji, lakini kwa hivi sasa tutapumua baada ya kuyaona maji katika mabomba yetu,” alisema Masha.
Naye Francisca Mbelwa, alisema wamekunywa maji ya chumvi kwa muda mrefu na kuyanunua kwa bei ya juu, hivyo sasa ni furaha kwa kuwa hawakuamini kama wangekumbukwa kutokana na kuwa walishakata tamaa ya kuona maji yakitoka kwenye kuta za nyumba zao.
“Tumekunywa sana maji ya chumvi yanayotoka kwenye visima, hapo mtu kama huna hela ya kununua maji kutoka kwenye magari inabidi uvumilie tu, lakini leo tumeambiwa haya maji yatakuwa yanatoka kwa saa 24 na yatakuwa yanauzwa kwa ndoo kubwa shilingi 100, tunaishukuru sana serikali na Dawasa kwa kutuletea maji,” alisema Mbelwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, alisema moja ya jukumu ambalo Rais John Magufuli amewatuma ni kusimamia na kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinafika kwa wananchi hasa wanyonge.
“Katika vitu vinavyokera katika jamii ni ukosefu wa maji pamoja na umeme na ndio maana serikali ya Rais John Magufuli ina sera ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani sambamba na kuhakikisha huduma za kijamii zinawafikia hasa watu wa chini," alisema Makori na kuongeza: "Sio kwamba baba haruhusiwi kuchota maji bali katika adha ya kutafuta maji mama anahusika kwa nafasi kubwa. Sisi wanaume ni hodari wa kufunga kanga na kwenda bafuni kuoga tu.
” ya maji iliyokuwa inawasumbua wananchi kwa muda mrefu. Meneja wa Dawasa Mkoa wa Ubungo, Mhandisi Pascal Fumbuka, alisema mradi wa mtaa wa Msakuzi utahudumia kaya 3,500 sawa na wananchi zaidi ya 200,000 na mpaka sasa wananchi zaidi ya 1,500 wamejitokeza kujaza fomu kwa ajili ya kuunganishwa na huduma hiyo.
“Tunatarajia kuongeza pato na kufikia shilingi bilioni 1.5 kwa mwezi na pia kupunguza wizi wa maji baada ya wananchi wa eneo hilo kuunganishiwa maji, kwa kuwa huduma ya kuunganishiwa maji wananchi ni ya mkopo na mteja ataingia mkataba na Dawasa ambapo utalipwa ndani ya mwaka mmoja,” Alisema Fumbuka na kuongeza:
"Katika Kata ya Kwembe Dawasa imejenga jumla ya vizimba vitatu kwa ajili ya kuhudumia wananchi wenye kipato kidogo, lengo kubwa ni kuhudumia wananchi hao wakati mwananchi mmoja mmoja akiunganishiwa maji na tumetoa maagizo ndoo ya maji itakuwa inauzwa shilingi 100 na tumeagiza kwa serikali ya mtaa asitokee mtu akauza maji juu ya bei hiyo.”