Maswali machache najiuliza;
Je wanapoyazuia watayafungua na kutafuta kujua kilichopo ndani?
Je hizo seal ziliwekwa baada ya Raisi kupiga marufuku au kabla?
Je kama ziliwekwa kabla kuna utaratibu gani wa kutenda haki?
Je kama ziliwekwa baada ni nani na nani wanahusika na watachukuliwa hatua gani?
Je kama huu usafirishaji wa mchanga upo kwenye mikataba ya uchimbaji kulikuwa na utafiti maalumu uliofanyika kabla ya uamuzi wa kusitisha usafirishaji huo? Na je tunajua ni nini kitafuata? Nchi haitaingizwa kwenye migogoro mingine isiyoisha kama ile ya kufua umeme?
Je nchi ilishatuma wapelelezi wake kwenye hicho kiwanda kinachopokea mchanga na kuthibitisha kuwa tunacholipwa kutokana na mchanga huo kinaendana na thamani yake?
Je ulifanyika uchambuzi yakinifu kuweza kukokotoa hasara itakayotokana na kusitishwa kwa usafirishwaji huo? kwa maana kujua gharama ya kusafirisha container mpaka migodini, kulijaza mchanga, kulisafirisha tena mpaka Dar, kulifanyia clearances, mikataba ya clearance and handling pale bandarini, malipo ya TRA, ukaguzi nk. upakiaji na upakuaji katika sehemu zote hizo, utunzaji wa hayo makontena kwenye yard zote hizo husika, mkataba na wasafirishaji kwa meli nk. nk...?
Tumefika hapa kwa sababu tumesaini mikataba ya madini isiyokuwa na tija kwa Taifa. Ndiyo maana Mwalimu aliwahi kusema kama hatujawa tayari kuyachimba ni afadhali tuyaache huko ardhini kuliko kukubali kudanganywa, unaonyeshwa kipande cha chupa unachekelea kama zuzu ukithania ni almasi.