Maselle na waziri wake amefanya jambo la kishujaa na kwa ushupavu mkubwa. Na ndicho tunachotaka sisi watanzania wa kawaida. Tatizo kubwa ni kwamba anaingia kwenye vita ambayo hajui adui ana uwezo mkubwa kiasi gani. Na pia hajui kuwa kwenye jeshi lake majemadari wote ni MAMLUKI wa adui. Tupigane maana ni lazima tupigane, ila kuishinda vita hii? Mmmmh! Mtandao wa wale jamaa ni mkubwa na una nguvu mno. Mnadhani kukwepa kodi kwa tanzaniteone kulikuwa hakujulikani miaka yote hiyo? Je kodi ni hiyo tu wamekwepa?