Greatguy
Member
- Nov 22, 2016
- 5
- 0
Novemba 22, 2016.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amezindua vyumba nane vya madarasa katika shule ya msingi Mbande, wilayani Temeke mkoani humo, ambavyo vitatu kati ya hivyo vimejengwa kutokana na fedha za Serikali zilizotolewa na Rais Dk. John Magufuli ili kupunguza changamoto ya vyumba vya madarasa mkoani humo.
Uzinduzi huo ameufanya ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake ya siku 10 kikazi mkoani humo, ili kusikiliza kero za wananchi wa wilaya zote tano na kuzitafutia ufumbuzi papo kwa hapo, kutokana na kuambatana na ujumbe wa watendaji wa idara zote za ofisi ya mkoa na wilaya husika.
Akiwa kwenye shule hiyo, ambayo ni miongoni mwa shule chache zenye wanafunzi wengi zaidi mkoani Dar es Salaam kwa kuwa na wanafunzi 5,551 Mkuu wa mkoa alisema licha ya uwepo wa idadi hiyo, Serikali iko makini kutengeneza mazingira mazuri kwa wanafunzi kujifunzia, ikiwemo kuongeza vyumba vya madarasa na kumaliza tatizo la uhaba wa madawati.
Makonda alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli, ilionyesha dhamira yake ya kuipa kipaumbele sekta ya elimu kwa kutangaza elimu bure ambayo wachache wasio na mapenzi mema na taifa, walibeza.
Alisema baada ya hapo, serikali iligeukia uhaba wa madawati uliotokana na ongezeko kubwa la uandikishwaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza katika mwaka uliopita wa masomo, ambapo shule zote nchini ikiwemo ya Mbande, uhaba wa madawati sasa ni historia.
Kabla ya kuzungumza na mamia ya wazazi waliofika shuleni hapo kumsikiliza, Makonda alizungumza na wanafunzi wa darasa la nne, ambao walitaja changamoto kubwa inayowakabili kuwa ni uhaba wa vyumba vya madarasa.
Wanafunzi hao walisema awali shuleni hapo kulikuwa na changamoto ya madawati tatizo ambalo halipo tena, hivyo walimuomba kiongozi huyo awasaidie kwenye utatuzi wa changamoto hiyo ili kuwa na mazingira mazuri ya kujifunzia.
Akijibu hoja hiyo pamoja na mambo mengine, Makonda alisema Serikali itaendelea kutekeleza wajibu wake lakini aliwaasa wanafunzi wawe wasikivu kwa walimu wao na wazazi ili elimu yao iwe na manufaa katika maisha yao.
“Mimi nimesoma kwenye shule za serikali kama nyie, nimepata shida kama nyie, nimetoka kwenye familia kama zenu, lakini kwa usikivu wangu mpaka sasa ni Mkuu wa Mkoa kwa hivyo usikivu ni jambo la msingi sana,” alisema.
Taarifa ya shule hiyo ilisomwa na Mwalimu Mkuu, Gaudence Mashaka, ambaye aliishukuru serikali kwa kumaliza changamoto ya madawati na kutaja changamoto zilizosalia kwenye shule hiyo kuwa ni uzio, ubovu wa vyumba sita vya madarasa, utoro wa wanafunzi, ukosefu wa ofisi ya walimu, uhaba wa walimu 53 na eneo dogo la shule.
Alitoa ombi kwa Mkuu wa Mkoa kujengwe shule mpya eneo la Mbagala Kisewe, ambako takriban wanafunzi 2,195 wa shule yake wanatoka maeneo hayo hivyo kukiwa na shule nyingine tatizo hilo litakwisha.
Kutokana na ombi hilo, Mkuu wa Mkoa aliagiza halmashauri ya Temeke na serikali ya mtaa kukaa na kuona namna ya kupata eneo la ujenzi wa shule mpya haraka iwezekanavyo ili wanafunzi wasome kwa nafasi na ufaulu uongezeke.
Alisema wakati serikali ikifanya hayo, wazazi wasiwakatishe tamaa wanafunzi na kwamba wawatie moyo na kuwalea katika maadili ili kuwaepusha na wimbi lola watoto wanaojihusisha na uhalifu kwa kuunda makundi likiwemo la Panya road.
“Wajibu wa kulea watoto ni la wazazi kwa kiasi kikubwa, nimemuagiza Kamishna Sirro, kama akimkamata motto wa miaka 17, akijihusisha na uhalifu wamtafute na mzazi wake atiwe ndani,” alisema.
Baada ya kumaliza jukumu hilo, msafara wake ulizuiliwa na wananchi kwenye soko la Mbande ambao walitumia fursa hiyo kutoa kero zao zikiwemo mgogoro wa matumizi ya eneo la soko na uwanja wa michezo, tatizo la ukosefu wa huduma ya umeme na gharama kubwa ya kupangisha vizimba vya soko hilo.
Kutokana na malalamiko hayo, Makonda aliwataka wakuu wa idara husika kutoa majibu sahihi kwa wananchi hao ambapo Meneja wa TANESCO mkoa wa Mbagala, alisema halifahamu suala hilo na kwamba atalithibitisha kisha kulifanyia kazi ndani ya wiki tatu kuanzia jana.
Kuhusu suala la mgogoro wa matumizi ya eneo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke alisema soko hilo bado limejengwa kutokana na uhitaji wa wananchi, ambapo mpaka sasa licha ya kukamilika limewekwa chini ya uangalizi wa wananchi na kwamba halmashauri bado haijaanza kutoza kodi.
Mkuu wa mkoa aliwahoji wananchi endapo wanataka soko hilo lihamishwe eneo lingine ili mahali lilipo sasa, pawe uwanja wa michezo na kituo cha basi, swali ambalo liliwagawa wananchi hao walioonekana wachache wakitaka iwe hivyo huku wengine wakitaka kuwe na mabadiliko.
Kutokana na mvutano huo, alitoa maagizo kwa Idara ya masoko ya halmashauri, kufuatilia suala hilo la soko ili kubaini mmiliki halali, gharama alizotumia kujenga, mapato anayoyapata na gharama za pango la kizimba kisha kuifikisha ofisini kwake kabla ya mwisho wa wiki hii.
Ziara hiyo iliendelea mpaka eneo la Chamazi, alikoenda kukagua eneo litakalojengwa kituo kikubwa cha polisi ambacho ni miongoni mwa vituo 20 vitakavyojengwa na Makonda kwa kushirikiana na wadau maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Mkuu wa mkoa majira ya mchana alizuru shule ya msingi Kiburugwa ambako aliweka jiwe la msingi ujenzi wa uzio wa shule hiyo katika mkakati wake wa kuboresha ulinzi na usalama wa wanafunzi mashuleni mkoani Dar es Salaam.
Pamoja na hilo, alikagua ujenzi wa kituo cha afya cha Kijichi pamoja na kuweka jiwe la msingi la kituo hicho kitakachohudumia idadi kubwa ya wananchi wa maeneo ya Mbagala Kuu na Kijichi, ambako alisema afya ni moja ya maeneo muhimu kwa maisha ya binadamu hivyo watendaji wanapaswa kusimamia vizuri miradi na kwa uaminifu.
Alasiri alifanya mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Zakhem, ambako mamia ya wananchi walijitokeza na kutoa kero zao.