Dar kugumu kweli

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
31,641
Reaction score
81,540
Jiji la Dar ni jiji ambalo kila mtu ambaye yuko mikoani anandoto yakuja kuliona nakujua liko vipi.

Sasa nawaasa wadau kuwa hili jiji sahivi nigumu sana endapo ukija huku unaweza kumezwa na jiji mpaka ukakosa mpaka nauli ya kurudi kwenu mkoani kumzika mama yako.

Kama unakuja Dar uje kwa malengo chanya maana kufanikiwa siku zote kupo tu ila cha muhimu nikuwa na subra kusali sana.

Kuhusu wanawake
Huku Dar wanawake wapo wakutosha yaani hata ukitaka kumiliki wachumba 30 unapata bila tatizo muhimu uwe na hela ya kutosha.

Ajira
Huku Ajira zipo japo mzee jiwe kavuluga maisha kwa kupandisha kodi.

Chakula
Huku chakula kipo ila ukipenda kula bila budget itakucost.

Hali ya hewa
Huku joto ni lakutosha unaweza kupigwa jua mpaka ukajuta kwanini ulikuja Dar.


Hitimisho;
Kama uko mikoani kuna fursa bora utulie huko huko maana sahivi mzee jiwe kavuruga kila sehemu naweza kuruka majivu ukakanyaga moto

Angalizo
Dar ni jiji lenye kila starehe uijuayo so yakupasa kuwa makini.
 
Miji mingine ingekuwa na maendeleo na fursa kama Dar, vijana wasingekimbilia jiji
 
lmao! next time andika kilugha tu
"chakura" cha dar lazima ukiote ukiwa kule kwetu "kulikobarikiwa" :-D
 
Nani wa kuishi kwenye mafuriko huko nyie pambaneni wote wangekuwa na ndoto za kuishi dar pasingetosha watu tulikuwa na ndoto za kufika Drovin Moscow Na London na tulifika halafu wewe unatutambia dar tu ambayo kila wiki tunaingia na kutoka acha tujenge mikoa yetu
 
Acha kuwatisha wenzio,waje tu kupambana! mbona maisha yapo kawaida tu.
 
sema maisha kwako magumu acha kutisha watu, kuna mtu alishawai kuja kukuomba nauli ya kurudia kwao??
 
maisha ya dar ni rahisi sana kwa kupata fedha ya kujikimu,ila sio pesa za maendeleo
 
eti Dar pagumu!we yaelekea huna exposure ya maisha ya nchi nyingine.nenda tu hata hapo Nairobi uone maisha magumu...Dar watu bado wanaishi maisha ya kijamaa,hakuna msoto wowote
 
Kwa mtu uliyekaa dar na unapajua vizuri sasa hivi ni mji wenye kerosana!....kama una issue nzuri nje ya dar Fanya tu huku unakuja siku mbili tatu ndo at least utaona dar nzuri!...sasa hivi mpango mikoani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…