Tatizo kufikiri kwetu kunafungwa na umasikini uliokithiri.
Ukweli ni kwamba kwa nchi ya Tanzania na rasilimali ilizonazo kikitokea chama, mfumo na watu binafsi wenye uelewa na uchungu wa kusimamia rasilimali hizi ni dhahiri zaidi ya 65% ya Watanzania watapanda juu ya mstari wa umasikini kwa muda usiozidi miaka tisa. Hii haitagemea mtu yuko Nangurukuru, Kyerwa, Nkasi, Chilonwa wala Buguruni Mnyamani.
Tukishaweza kuiweka 65% juu ya mstari wa umasikini basi ni wazi katika hao wamiliki wa magari watakuwemo badala ya kutegemea wamiliki wawe wanasiasa na wezi serikalini. Kwa maana hiyo miji yote itakuwa na uwezekano wa kukua kwa maana hivi sasa mfumo wa rushwa ndio unafanya watu wengi wajirundike Dar es Salaam. Kama alivyowahi kusema Mwalimu kuwa serikali corrupt inatumikia matajiri na matajiri uchwara wote wanaioshi Dar es salaam.
Mtu anayelipwa billion 60 kushona uniforms za taasisi lakini akala pesa zote bila kufanya lolote 99% ya watu hao na makuwadi wao wanaishi Dar es Salaam. Hii inaweza kubadilisha mambo.