Dalili za upungufu wa maji mwilini

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
DALILI ZA UPUNGUFU WA MAJI MWILINI

Upungufu wa maji mwilini ni hatari. Dalili zinazoweza kujitokeza ni pamoja na:

  • Kukojoa mkojo wa njano nyeusi
  • Kuumwa na kichwa
  • Mwili kukosa nguvu
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Kiu
  • Mdomo na ulimi mkavu (unapogusa ndani ya shavu la mgonjwa, unahisi pakavu)
  • Kukojoa mara chache na mkojo ukiwa na rangi nzito
Unapobaini dalili hizo, anza tiba mara moja kabla hali haijawa mbaya zaidi.

Dalili zinazoonesha upungufu mkali wa maji mwilini
  • Udhaifu mwili mzima: uchovu,kukosa nguvu, usingizi nk
  • Mapigo ya moyo kwenda haraka
  • Pumzi nzito
  • Macho kuingia ndani yasiyo na machozi
  • Ngozi inapofinywa kubaki katika hali hiyo ya kufinywa
400px-NWTND_bag_Page_20-2.png

Vuta ngozi katikati ya vidole viwili kama kwenye mchoro... kama ngozi haitarudi katika hali yake ya kawaida, huenda mtu huyu ana upungufu mkali wa maji mwilini.
  • Miongoni mwa watoto wachanga, shimo laini juu ya kichwa

Ili kujiepusha na matatizo ya upungufu wa maji na hatimaye kujikuta unakumbwa na dalili kadhaa zilizoelezewa hapo, ambazo ziko pia kwa watu wazima wengine, ni kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Hata utakapozidiwa na kukimbizwa hospitali, hakuna dawa nyingine utakayopewa zaidi ya maji (re-hydrating solution). Kwa nini usubiri hali hiyo ikutokee wakati unaweza kuizuia kwa kunywa maji tu?

Epuka vinywaji ambavyo huzidisha upungufu wa maji mwilini
120px-NWTND_bag_Page_23-2.png

Hapana!
Vinywaji vilivyokolezwa sukari,vinywaji vyenye kemikali ya kafini (caffeine), na pombe huzidisha tatizo la upungufu wa maji mwilini. Hivyo epuka:

  • Soda (Coke, Fanta, Pepsi) na vinywaji vingine vilivyokolezwa sukari.
  • Kahawa na chai iliyokolea sana.
  • Biya, mvinyo na pombe zingine.
 
Back
Top Bottom