Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,881
Dah.
Hii nimeisoma kwenye katiba ya chadema. Kumbe chama hiki kinaweza kikavunjwa na watu kugawana mali. Duh! Hebu check hii hapa
9.4 Kuvunjwa kwa Chama
Sasa hii issue inaweza ikawaaumiza sana hawa Chadema. Maana hawa wadhamini wao akina Lowassa wanaweza wakashawishi robo tatu na kufanya chama kivunjike ili wapate mshiko.

9.4.1 Chama kitavunjwa rasmi endapo robo tatu (3/4) ya wajumbe wote watakaohudhuria Mkutano Mkuu wa Chama wa Taifa ulioitishwa kwa madhumuni ya kuvunjwa kwa Chama watapitisha hoja hiyo. Mkutano huo utatangaza rasmi kuvunjwa kwa Chama na kusimamishwa kwa shughuli zote za Chama.
9.4.2 Katika tukio la kuvunjwa kwa Chama, bodi ya wadhamini wa Chama itahodhi mali hiyo kulipia madeni yote ya Chama. Endapo kutakuwa na salio lolote la mali ya Chama baada ya kulipa madeni yote, salio hilo litawasilishwa au kukabidhiwa kwa taasisi yoyote inayoshughulikia wasiojiweza ama Chama chochote cha wasiojiweza Tanzania kwa jinsi itakavyoamuliwa na bodi ya wadhamini.
9.4.3 Katika tukio la kuvunjwa kwa Chama kwa nia ya kuungana na Chama kingine cha siasa bodi ya wadhamini wa Chama itahodhi mali yote ya Chama na kuitumia mali hiyo kulipia madeni yote ya Chama. Endapo kutakuwa na salio lolote la mali ya Chama baada ya kulipa madeni ya Chama salio hilo litatumika kufuatana na azimio la kuvunja Chama ili kuungana na Chama kingine.